PROFESA MUHONNGO NI MTU MWENYE HULKA YA KUSEMA UONGO, NI VITA YA MANENO KATI YAKE NA REGINALD MENGI KATIKA ISHU YA GESI.
REGINALD MENGI.
DAR ES SALAAM.
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP,
Reginald Mengi amesema kauli zinazotolewa na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo dhidi yake kuhusu uwekezaji katika
sekta ya gesi nchini hazina ukweli wowote.
Prof. Sospeter Muhongo.
Mengi jana alitoa taarifa yake katika
vyombo vya habari na kueleza kuwa waziri huyo ni mtu mwenye hulka ya
kusema uongo, kauli ambayo ameitoa ikiwa zimepita siku mbili tangu
waziri huyo kudai kuwa Mengi anamiliki vitalu vingi vya gesi, kwamba
anataka kupewa upendeleo wa kupewa wakati hawezi kuviendeleza.
Huku
akitaja mambo kadhaa ya uongo kuhusu waziri huyo, Mengi
alisema,“Sikutegemea kama Muhongo ataendeleza vita dhidi yangu. Mtu huyu
ana hulka ya kusema uongo, amewahi kuwaahidi Watanzania kuwa hakutakuwa
na mgawo wa umeme, lakini upo mpaka sasa.”
Alisema
hamiliki migodi mingi ya madini kama inavyodaiwa “Ukweli ni kwamba, mimi
namiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa
madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba.”
Alifafanua, “Muhongo anafahamu kwamba kuna aina sita za leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini.
Lakini
kwa makusudi kabisa anafananisha leseni ya Mtanzania anayetafuta au
kuchimba kokoto na leseni ya mwekezaji wa kigeni anayetafuta au kuchimba
urani au dhahabu. Kweli unaweza kufananisha kokoto na dhahabu.”
Alisema
kuwa licha ya kuwa utafutaji wa madini ndiyo husababisha watu kugundua
eneo lenye madini, kuanzia Julai mwaka jana Waziri Muhongo amepandisha
tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na 500 na kusababisha Watanzania
wengi kurudisha leseni zao. MWANANCHI

No comments:
Post a Comment