Header Ads

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema baadhi ya mawaziri wamekuwa wakaidi kufuata ushauri wa kisheria ambao amekuwa akiutoa na kwamba hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayotokea katika utendaji wa Serikali, yakiwamo yale yaliyobainika katika Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.  
---
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema baadhi ya mawaziri wamekuwa wakaidi kufuata ushauri wa kisheria ambao amekuwa akiutoa na kwamba hicho ndicho chanzo cha matatizo yote yanayotokea katika utendaji wa Serikali, yakiwamo yale yaliyobainika katika Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili.
Wakati Jaji Werema akiwananga mawaziri, kwa upande mwingine amemsifia Rais Jakaya Kikwete akisema kuwa yeye si kama mawaziri wake kwani ni msikivu na anayeshaurika. Akizungumza na mwandishi wetu jana, Jaji Werema alisema endapo ushauri ambao amekuwa akiutoa mara kadhaa kwa mawaziri ungezingatiwa, kilichotokea bungeni mwishoni mwa wiki cha mawaziri kung’oka kisingekuwapo.
“Tunatakiwa kuiga msemo wa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema kuwa ‘tii sheria bila shuruti’, Rais tunamshauri na anashaurika kwa nini mawaziri wakatae kuzingatia ushauri?” alisema Werema na kuongeza:

 “Mawaziri hawatakiwi kujifanyia tu mambo yao. Tunawaandikia barua lakini zinakwenda na yanafanyika yaleyale... Hata mimi nikionekana kukiuka sheria na kanuni naweza kuwajibishwa kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.”Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........

No comments:

Powered by Blogger.