JENERALI MSTAAFU WAITARA APOKEA WAPANDA MLIMA WA ‘UHURU EXPEDITION’ NA KUWATUNUKU VYETI
…………………………………………………………………………………………
Na Geofrey Tengeneza
Aliyekuwa
Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania-JWTZ Jenerali mstaafu
George Waitara ameihakikishia Bodi ya Utalii Tanzania –TTB kuwa Jeshi
hilo litaendelea kuunga juhudi za TTB katika kuvitangaza vivuto vya
Utalii vya Tanzania ukiwemo mlima Kilimanjaro kupitia msafara wa kupanda
mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la Uhuru Expedition unaofanywa na Jeshi la Wananchi kila mwaka katika kuadhimisha Uhuru wa Tanzania.
Jenerali Waitara ambaye ndiye Kiongozi na msimamizi mkuu wa Uhuru Expedtion aliyasema
hayo jana wakati akiwapokea wapanda mlima walioshiriki katika msafara
huo mwaka huu ulioratibiwa na kufadhiliwa na Bodi ya Utalii Tanzania
katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro –KINAPA Marangu Moshi.
“Tunaishukuru sana Bodi ya Utalii kwa kushirikiana nasi kwa mara
nyingine tene katika msafra huu, lakini pia nawashukuru sana KINAPA kwa
msaada wote waliotupa na niwahakikishie kuwa Jeshi litaendelea
kuutangaza utalii wetu wa Tanzania ukiwemo utalii wa kupanda mlima
Kilimnjaro” alisema Jenerali msataafu Waitara ambaye pia aliwakabidhi
vyeti wapanda mlima sita.
Mapema
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Balozi Charles Sanga ambaye
pia alikuwa miongoni mwa wapanda mlima alisema kuwa Bodi ya Utalii
inafurahi kuona kuwa Uhuru Expeditioniliyoasisiwa
na Jeshi la wananchi wa Tanzania inaendelea kuimarika na kutekeleza
malengo ya kuanzishwa kwake na kwamba kwa kutambua mchango wa Expedition hii ndiyo maana TTB imekuwa ikiiunga mkono. Amemsifia Jenerali Waitara kwa kuisimamia vema Expediton hii na kwa juhudi zake za kuhakikisha kila mwaka tukio la kupanda mlima la Uhuru Expedition linafanyika.
Naye
Kiongozi wa Msafara uliopanda mlima mwaka huu Meja Jenerali Christopher
Gimongi amesema msafara huu uliokuwa na wapanda mlima saba ulianza
kupanda mlima tarehe 6/12/2013 kupitia njia ya Marangu na kwamba ni
wapanda mlima watatu tu akiwemo yeye walioweza kufika kileleni. Meja
Jenerali Gimongi alisisitiza umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kufadhili Uhuru Expedition kama alivyoahidi Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki wakati wa tukio kama hilo kama mwaka jana.
Tukio la kupanda mlima mwaka huu kupitia Uhuru Expedition lilishirikisha
wafanyakazi wawili wa TTB, Mwenyekiti wa TTB baolzi Charles Sanga, Meja
Jenerali Mstaafu Christopher Giomongi na wafanyakazi watatu kutoka
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akiwemo mwanamke mmoja.
No comments:
Post a Comment