WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AANZA ZIARA KATIKA MKOA WA MOROGORO KWENYE MIRADI YA UMEME
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na watendaji wa shirika
la umeme nchini (Tanesco) ikiwa ni pamoja na wadau wa umeme mjini
Morogoro kabla ya kuanza rasmi ziara yake kwenye miradi ya umeme.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa meneja
wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba mara baada ya kujionea
moja ya transfoma iliyojengwa kwa ajili ya kupeleka umeme katika kijiji
cha Matombo kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
Kazi
ya kuweka umeme ikiwa ni pamoja na kufunga mita ikiendelea kwenye moja
ya nyumba zilizopo katika kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya ya
Morogoro Vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya umeme.
Meneja wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba akitoa ufafanuzi
wa maendeleo ya miradi ya umeme katika kijiji cha Mtombozi mbele ya
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na mmoja wa
wakazi wa kijiji cha Ngong’oro kabla ya kusikiliza kero zao ikiwa ni
pamoja na kuzungumza nao
Mwenyekiti wa kijiji cha Ngong’oro Mahamba Shukuru akiwasilisha changamoto katika upatikanaji wa huduma ya umeme katika kijiji hicho kwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambapo Waziri huyo ameahidi kufanyia kazi mara moja kupitia kwa watendaji wake.
No comments:
Post a Comment