Wazazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mzee Kabwe Zuberi na
Shida Salum. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, jana
alisindikizwa
na wazazi wake jana pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi
kipya
katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari aliouitisha baada
ya kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho. Tangu alipoanza
kupata umaarufu katika medani ya siasa, mbunge huyo hajawahi kuonekana
hadharani akiwa na baba yake mzazi, Zuberi Kabwe, bali mama yake Shida
Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
No comments:
Post a Comment