Header Ads

WABUNGE WA EALA KUTOKA TANZANIA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE, WASISITIZA MAZUNGUMZO KUTATUA MIGOGORO


WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji.
Kimbisa akizungumza na wanahabari Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo..
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji. Kulia ni Mkurugezni Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam Kimbisa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo pia alipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu ya Jumuiya hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.