VIONGOZI WA SHIRIKA LA MISAADA LA HANNS SEIDEL FOUNDATION WAMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHINI DK. NCHIMBI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
(kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika
la Misaada la Hanns Seidel Foundation, Dk. Peter Witterauf. Kulia ni
Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert. Viongozi wa Shirika
hilo kutoka Makao Makuu, Kanda ya Afrika pamoja na Mwakilishi Mkazi
wa shirika hilo nchini walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake jijini
Dar es Salaam leo kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
wizara yake na shirika hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada
la Hanns Seidel Foundation masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
wizara yake na shirika hilo. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
shirika hilo, Dk. Peter Witterauf, anayefuata ni Mkuu wa shirika hilo,
Kanda ya Afrika, Klaus Liepert, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo
nchini Tanzania, Konrad Teichert. Viongozi wa Shirika hilo lenye Makao
Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani walimtembelea Waziri Nchimbi
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
(wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika
la Misaada la Hanns Seidel Foundation. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa shirika hilo, Dk. Peter Witterauf, wa pili kulia ni Mkuu wa shirika
hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa
Shirika hilo nchini, Konrad Teichert na kulia ni Naibu Kamishina wa
Polisi Makao Makuu, Tathimini na Ufuatiliaji, (DCP) Omar Rashid. Viongozi
wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani
walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na Shirika
hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment