RAIS KIKWETE KUWA MIONGONI MWA VIONGOZI MBALIMBALI WATAKAOPEWA TUZO ZA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO
NOVEMBA 23, mwaka huu, viongozi mbalimbai watapewa tuzo za kutambua
mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto.
Tuzo
hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madaktari Waliosoma Vyuo Vikuu nchini
(THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu
ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na Mwenyekiti wa
makampuni ya IPP, Reginald Mengi
Kuhusu THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini
wakiwa wengi, watahudumia watu wengi na jamii kubwa zaidi. Anasema, hadi
sasa taasisi ina madaktari wanachama zaidi ya 120 ambao wamesambaa
nchi nzima. "Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha
uboreshaji huduma za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa
huduma bora za afya kwa watanzania,"anaongeza. Madaktari hao ni wale
walioamua kubaki nchini badalayakukimbilia nje
ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.
"Tuliamua kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri zaidi
kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu. "Dira ya taasisi yetu, tunaona
watanzania wenye afya bora, huduma bora , na miundombinu bora katika
kutoa huduma za afya nchini . Katika taasis yetu nguvu yetu ni umoja;
wote ni sawa, kila mtu ni muhimu na kila mtu ni kiongozi. Nguvu yetu
ni matumaini,"anaongeza.
Dk. Kyaruzi anasema ili kuwa na madaktari wengi sehemu mbalimbali nchini
wanaotoa huduma za afya, taasisi imeanzisha Idara ya Uendelezaji
Madaktari Vijana inayoratibu Mtandao wa Madaktari Vijana Nchini, ambao
ni Madaktari Wanafunzi( Medical Students), Intern Doctors, na Madaktari
wanaoanza kazi ili kuwajengea uwezo kitaaluma. Aidha, katika kutatua matatizo ya afya nchini, anabainisha kuwa wanaongozwa na mpango mkakati.
Katika
mpango wa mwaka 2011/2014, taasisi imejielekeza katika kutekeleza
malengo ya Milenia, lengo la nne na tano, afya ya mama na mototo. Na
kufikia lengo la kupunguza vifo vya akina mama kwa 75% ifikapo mwaka
2015. Katika kutekeleza jukumu hili muhimu, taasisi imeanzisha kampeni
ya kitaifa ya Saidia Mama Mjamzito Ajifungue salama, ili kupunguza vifo
vya mama na mtoto.
Kutokana na taarifa za jarida la umoja wa mataifa , Global Health and
Deplomacy, duniani kina mama wajawazito 368,000 wanafariki kila mwaka,
nafasi ya mama mjamzito kufa ni mara 100 zaidi katika nchi zenye
idadi kubwa ya vifo vya akina mama vinavyotokana na ujauzito. Akifafanua
hilo, Dk. Kyaruzi anasema kuwa ni nchi 21 tu duniani ziko kwenye hatua
sahihi katika kufikia malengo ya millennia ifikapo mwaka
2015. "Vifo vya mama wajawazito nchini kwa mwaka 2005 vilikuwa ni 578, kwa vizazi hai 100,000, na kufikia 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment