MAMA TUNU PINDA ATOA MSAADA WA VIATU PEA SITINI KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA KATANDALA (MARTIN DE PORES) SUMBAWANGA MKOANI RUKWA
Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akimkabidhi Sister Scholastica Mwembezi wa
Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha
kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa viatu pea sitini zilizotolewa
na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda
ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea kituo hicho mapema mwaka huu.
Aidha Sister Mwembezi amemuomba Katibu Kanyanda kumfikishia salamu za
shukrani Mama Pinda ikiwa ni pamoja kumkumbusha ahadi ya gari aliyoitoa
kwa kituo hicho.
Ndugu
Charles Kanyanda akimvisha viatu mmoja ya watoto yatima katika kituo
hicho baada ya kukabidhi zawadi hizo kutoka kwa Mama Tunu Pinda. Mzee
Kanyanda amewataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo wa upendo katika
kusaidia mahitaji mbalimbali kwa watoto na kituo hicho.
Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akiimba moja ya wimbo na watoto wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment