KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI TUNDURU KWA KISHINDO,KESHO KUANZA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA.
Msimamizi
wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho
zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na
Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli
mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.
Maeleoz
yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa
na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na
wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa
ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo
kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
Katibu
wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama
wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho
Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira
wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Baadhi
ya akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha
Korosho Africa,wakiendelea na kazi yao ya kuchambua Korosho,ambapo
imeelezwa kuwa mtu mmoja huchambua korosho kwa wastani wa kilo kumi
mpaka 15.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza
na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha
Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo
na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.
Tahadhari ya maandishi ndani ya kiwanda cha Korosho kwa wafanyakazi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa tarafa
ya Jakika mapema leo mchana,ikiwa sambamba na kuweka jiwe la msingi
kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Jakika,Wilayani Tunduru mkoani
Ruvuma,Ndugu Kinana ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi nje ya
Zahanati ya kijiji cha Matemanga,Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi
nyumba mbili za Waganga ikiwemo na kushiriki ujenzi wa mradi wa nyumba
hizo akiwa sambama na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Moja ya nyumba za watumishi wa Zahanati ya kijiji cha Matemanga ambayo Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi.
Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana sambamba na ujumbe wake Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,wakishiriki ujenzi wa nyumba mbili za Waganga katika zahanati ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvumma.
Baadhi ya akina mama wakifurahia jambo wakati Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake
Wilaya ya Tunduru mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la
Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini wakishangilia jambo wakati Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake
mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na
kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihitimisha
ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na
kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho
ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya
Wananchi na chama kwa ujumla.
Baadhi
ya Mafundi wakiendelea na ujenzi kwenye moja ya darasa ikiwe ni sehemu
ya mradi wa ujenzi wa madarasa na maabara katika shule ya sekondari ya
kata ya Mgomba,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana
na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro walishiriki ujenzi -
Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiishiriki ujenzi kwenye
moja ya darasa ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa madarasa na
maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Mgomba,iliopo Wilaya ya
Tunduru mkoani Ruvuma.Anaeshuhudia ni Mkoa wa Ruvuma,Mh Said Thabit
Mwambungu.
No comments:
Post a Comment