Header Ads

KITUO CHA KISUKARI CHA ST. LAURENT DIABETES CENTRE CHA ZINDULIWA RASMI

 Muuguzi katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre, akimpima Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ask. Dk. Alex Malasusa huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akishuhudia.
 Wananchi mbalimbali wakipata huduma ya kupimwa ugonjwa wa sukari katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre
Burudani kutoka Mjomba Band ikitolewa
******
Ugonjwa wa Kisukari umekuwa tishio kwa mataifa mengi duniani, Tanzania ikiwemo. Inasemekana kuwa nchi maskini na zinazoendelea duniani ndio zinazongoza kwa ugonjwa wa Kisukari. Aidha, kwa sasa ugonjwa wa Kisukari unashika nafasi ya tatu duniani kueneza vifo.

Katika makala hii, Mtaalam  wa Maradhi  ya Kisukari , Dkt. Mary Mayige , kutoka kituo cha Kisukari cha St. Laurent Diabetes Centre, jijini Dar es Salaam anaeleza kwa ufasaha dalili za ugonjwa huu, kinga na tiba yake.

Dkt. Mary Mayige  anafafanua kuwa Kisukari kwa kifupi (na kwa lugha ya kueleweka) ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari kwenye damu.  Aliongezea kuwa sukari inapokuwa nyingi kwenye damu ya binadamu, hapo ndipo mtu huyo husumbuliwa na maradhi hayo.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo cha Kisukari yaani St. Laurent Diabetes Centre, Dkt. Mary Mayige aliwakaribisha watanzania wote katika upimaji wa bure wa Kisukari na pressure katika kituo chao kilichopo Msasani karibu na CCBRT, Dar es Salaam tarehe 10/11/2013. Kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho, watanzania walijitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao siku hiyo na kujipatia ushauri wa bure kutoka kwa madaktari na wauguzi wa kituo hicho.

Watu wengi walinufaika na huduma zilizotolewa na kitu hicho cha St.Laurent Diabetes Centre.

Siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani, kituo cha St. Laurent Diabetes Centre walifanya uzinduzi rasmi wa kituo chao Wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Alex G. Malasusa, pamoja na Waziri  wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt .Hussein Mwinyi, na  Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba na waheshimiwa wageni waalikwa wawakilishi kutoka serikalini, kwenye  sekta binafsi , za umma na sekta za afya.

No comments:

Powered by Blogger.