Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na bastola inayodaiwa kuwa ilikuwa inamilikiwa na marehemu Dk Sengondo Mvungi.

            
Kamanda wa Polisi Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova 
akiwaonyesha waandishi wa habari bastola iliyodai ni ya Marehemu Dk 
Sengondo Mvungi, ambayo polisi wamedai wamemkamata nayo mkazi wa 
Kiwalani katika eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
PICHA|PAMELA CHILONGOLA
----- 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
 linamshikilia mtu mmoja (jina tunalihifadhi), kwa tuhuma za kukutwa na 
bastola inayodaiwa kuwa ilikuwa inamilikiwa na marehemu Dk Sengondo 
Mvungi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, 
Kamishna Suleiman Kova alidai jana kuwa mkazi huyo wa Kiwalani, Dar es 
Salaam alikutwa na bastola aina ya Revolver yenye namba BDN 6111 ikiwa 
na risasi 21 na baada ya kufuatilia kumbukumbu zao na kuwasiliana na 
familia ya Dk Mvungi walibaini kwamba ilikuwa ni ya mwanasheria huyo 
nguli.
                
              
Huyo anakuwa mtuhumiwa wa 10 kukamatwa tangu 
kutokea kwa tukio la kushambuliwa kulikosababisha kifo cha Mjumbe huyo 
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
                
              
Dk Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba 
Msakuzi, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Novemba 3, mwaka huu. Mbali ya 
kushambuliwa, wavamizi pia waliiba bastola, kompyuta mpakato (laptop) na
 simu tano za mkononi.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea......
No comments:
Post a Comment