Airtel, Baraza la Taifa la Usalama barabarani waungwa mkono na wananchi
Naibu
Waziri wa mambo ya ndani, Bw. Pereira Silima (wa kwanza
kushoto)akizungumzia umuhimu wa kupambana na ajali za barabarani leo
katika hafla fupi ya kumtangaza Athmani Hamisi (wa tatu kutoka
kulia)kuwa balozi wa usalama barabarani iliyofanyika katika ukumbi wa
habari maelezo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Airtel Money
Asupya Nalingigwa akifuatiwa na Mjumbe wa baraza la taifa la usalama
barabarani Bw. Yakubu Rajabu.
Naibu
Waziri wa mambo ya ndani, Bw. Pereira Silima (katikati) akisisitiza
jambo juu ya umuhimu wa kila mwananchi kutii sheria bila shuruti ili
kuepusha ajali za barabarani wakati wa hafla fupi ya kumtangaza Athmani
Hamisi (kulia)kuwa balozi wa usalama barabarani iliyofanyika katika
ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kamanda Mkuu
wa Jeshi la Polisi DCP Mohamed Mpinga.
Aliyeteuliwa
kuwa balozi wa kampeni ya nenda kwa usalama barabarani, Bw. Athmani
Khamisi akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya
kutangazwa rasmi kuwa balozi wa kampeni ya nenda kwa usalama barabarani
iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la habari maelezo jijini Dar es
salaam hivi karibuni.Kulia kwake ni Mjumbe wa baraza la usalama
barabarani Bw. Yakubu Rajabu.
BAADHI
ya wananchi wanaoishi jijini Dar es salaam wamesema uamuzi uliofikiwa
na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kumtangaza aliyekuwa mpiga
picha wa magazeti ya serikali Bw. Athmani Hamisi kuwa balozi wa kampeni
ya usalama barabarani una maana kubwa sana.
Wananchi
hao wameyasema hayo katika nyakati tofauti walipokuwa wakihojiwa na
mwandishi wetu juu ya kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani
inayodhaminiwa na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel.
Wananchi
wengi wamesema uamuzi huo wa kumteua Bw. Hamisi kuwa Balozi wa kampeni
hiyo kwa dhumuni la kutoa elimu ya usalama barabarani utakuwa na matunda
zaidi kwa sababu kupitia yeye watu watajifunza vyema juu ya athari za
ajali barabarani.
“Kumtumia
mtu ambaye alishakuwa muhanga wa ajali ni jambo sahihi kabisa kwa
sababu ataweza kutoa ushuhuda wa wazi ni jinsi gani ajali zimemkwamisha
hata kwenye shughuli zake za kimaendeleo na kuwaasa vyema watu
wanavyotakiwa kujikinga na ajali hizo.” Alisema Calisti Mushi mkazi wa
Temeke jijini Dar es salaam.
Kwa
upande mwingine baadhi ya wakazi wa sehemu mbalimbali za jiji la Dar es
salaam walisema ni kweli kuwa jukumu la kupinga ajali ni la kila
mwananchi lakini elimu zaidi inapaswa kutolewa ili kuzitokomeza kabisa.
“Bado
elimu inahitajika zaidi kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuepusha
ajali ambazo hutokea kila siku, na kwa kutumia wahanga wa ajali kama Bw.
Hamisi watu wataelewa vizuri zaidi ni jinsi gani ajali hudumaza
maendeleo ya taifa kiujumla” walisema baadhi ya wananchi waishio katika
jiji la Dar es salaam.
Kwa
upande wake Balozi huyo mpya wa kampeni ya usalama barabarani, Bw.
Hamisi alisema atajitaidi kwa hali na mali kutoa elimu na kuwaasa
wananchi kuwa makini wanapokuwa njiani kwani ajali zinazotokea
hukwamisha maendeleo kwa kiasi kikubwa.
“Mimi
binafsi nimepumzika kwa muda mrefu kutokana na ajali niliyoipata, nataka
nitumie fursa hii kama balozi kuiasa jamii na kutoa elimu juu ya
madhara ya ajali na nini tufanye ili tuweze kuziepuka” alisema Hamisi.
Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema Airtel haitoacha kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na Baraza la taifa la usalama barabarani
katika kuokoa maisha ya watanzania ambayo hupotea kutokana na ajali za
barabarani.
“Tunatambua
umuhimu wa kuepusha ajali za barabarani na ndio maana tunaiunga mkono
kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha vifo
na majeruhi ambavyo hupatikana mara nyingi kwa kutokuwa na elimu ya
usalama barabarani,” alisema Mmbando.
Kampeni
ya nenda kwa usalama barabarani ina dhumuni la kutoa elimu kwa wananchi
juu ya sheria za barabarani na itafanywa katika mikoa mbalimbali
nchini.
No comments:
Post a Comment