Header Ads

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MASANDUKU YA MAONI.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa Amani Mwamwindi wa saba kutoka kulia (waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja  na wajumbe wa walimaliza muda wao wa Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Iringa.
 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa Amani Mwamwindi akimkabidhi barua ya shukrani aliyekuwa mmoja ya wajumbe wa Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya Vitus Mushi na diwani wa kata ya mtwivila mara baada ya kuvunja bodi hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Iringa. (Picha zote na Denis Mlowe)
======  ======  ======
WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MASANDUKU YA MAONI.
Na Denis Mlowe,Iringa
WANANCHI wameshauriwa kutosubiri mikutano kutoa maoni yao kuielekeza serikali matatizo ambayo yanaweza kutatulika kabla ya mikutano kwa kutuma maoni katika masanduku ya maoni yaliyoko katika zahanati, vituo vya afya na Hospitali.
Akizungumza wakati wa kuvunja Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya Afya, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa Iringa Amani Mwamwindi alisema imekuwa kasumba ya wananchi wengi kutoa malalamiko katika mikutano ya hadhara ambayo huchukua muda mrefu kufanyika tofauti na masanduku ya maoni ambayo yanapatikana katika vituo hivyo.
Alisema mwananchi anaruhusiwa kutoa maoni yake kama hajaridhika na huduma apatayo katika sehmu husika na kuwataka wanakamati wa bodi za vituo hivyo kufutialia kwa ukaribu malalamiko ya wananchi katika kupata huduma bora.
Mwamwindi alisema bodi hizo zimeuundwa kwa ajili ya kuendeleza halmashauri katika kutoa huduma bora kwa wananchi wake katika sekta ya afya hivyo ni jukumu la kila mmoja kutambua bila afya bora kwa wananchi ni sawa na hakuna kitu kinachoweza kufanyika.

No comments:

Powered by Blogger.