Mkuu wa mkoa wa Mwanza kushiriki Rock City Marathon 2013
Afisa
Michezo Jiji la Mwanza Bw. Mohamed Bitegeko (kulia) akipokea fomu ya
usajili kutoka kwa Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza, Bw. Peter
Mujaya, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za
kilometa tano (5) za mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba
,2013 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Afisa
Michezo Jiji la Mwanza Bw. Mohamed Bitegeko (kulia) akipokea jesi ya
kukimbilia ambayo itatumika mwaka huu katika mbio za Rock City Marathon, kutoka kwa Meneja Biashara wa Airtel katika kanda ya Ziwa Bw. Raphael Dandi, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za
kilometa tano (5) za mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba
,2013 katika uwanja wa CCM Kirumba.
====== ======= =======
Mkuu wa mkoa wa Mwanza kushiriki Rock City Marathon 2013
SIKU
chache baada ya kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon 2013
kutangaza usajili rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo
ametangaza kushiriki mbio hizo kutokana na umaarufu wake maeneo mengi
Kanda ya Ziwa.
Mbio
hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba ,2013 katika uwanja wa CCM
Kirumba na tayari watu wengi wameanza kuchukua fomu ili kushiriki.
Ndikilo
alitangaza ushiriki wake jana katika hafla fupi ya uzinduzi wa Rock
City Marathon 2013 kanda ya ziwa yenye lengo la kuhamasisha wananchi
wengi kujitokeza mwaka huu.
Ndikilo
ambaye aliwakilishwa na, Afisa Michezo Jiji la Mwanza Mohamed Bitegeko,
mbali na kuipongeza kampuni ya Capital Plus International ambayo ni
mwaandaji wa mbio hizo, alitoa wito kwa viongozi wa chama cha Riadha
Mkoani Mwanza, waratibu na wasimamizi wa michezo wilayani na Mkoa wa
Mwanza kuongeza nguvu katika kuhamasisha ushiriki wa watu ili mkoa huo
uweze kuvumbua na kuinua vipaji vipya katika riadha.
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), African Barrick Gold, Precision Air, Airtel, Bank M, Parastal
Pensions Fund (PPF), Nyanza Bottlers, New Mwanza Hotel, Sahara
Communication na Umoja Swithch ambao wamejitokeza kuunga mkono jitihada
hizi ambazo zitasaidia kuinua mchezo wa riadha nchini pamoja na
kutangaza nchi yetu,” alisema.
Aliagiza
viongozi wa michezo na utamaduni wa Mwanza kuitumia fursa inayoletwa na
mbio hizo ili kutangaza mkoa wa Mwanza, na Tanzania kwa jumla
kimataifa.
“Tumeshuhudia
wanariadha mbali mbali vijana wa nchi kama Kenya wakiibuka washindi
katika mbio zilizofanyika mjini Berlin, Ujerumani hivi karibuni na
kujinyakulia fedha nyingi pamoja na zawadi mbali mbali. Hii iwe chachu
kwetu kama mkoa na Taifa kwa ujumla kutilia mkazo mchezo huu kwani licha
ya kuwa ni ajira kwa vijana lakini pia zinatumika kama kitambulisho
kikubwa cha taifa letu kimataifa endapo wanariadha wetu wataweza kufanya
vizuri,” alisema Ndikilo.
Nae
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza Silas Nkungu alisema mbiyo
za Rock City Marathon imeleta hamasa kubwa katika mkoa wa Mwanza hasa
kwa kuitangaza kimichezo na kuongeza kuwa kwa mwaka huu, Mwanza imeshika
nafasi ya nne kitaifa katika michezo.
Mratibu
wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema tofauti na mwaka jana, kwa mwaka
huu washiriki wataweza kujisajili kupitia Airtel Money na kuongeza kuwa
fomu zitapatikana kwenye maduka yote ya Airtel.
“Kwa
wale watakao tumia Airtel Money kujisajili, unapaswa kutuma pesa kwa
jina la fumbo (MARATHON) ambapo utapokea ujumbe utakaouonyesha pale
utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu ya
Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza,”
alisema.
Kasonta
aliongeza kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata
fomu zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika
ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu,
upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.
Alibainisha
kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo;
shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa
mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi).
Alisema
kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu
wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa
miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.
No comments:
Post a Comment