mafunzo kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wafunguliwa leo
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.
George D. Yambesi akifungua mafunzo kwa Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za
Kiutumishi na Mishahara .
Mmoja kati ya washiriki, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimajanro Dtk
Faisal Issa akiongea kuhusu mafunzo hayo, na kutoa shukrani.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi.
KILICHOJIRI KATIKA OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI, MAJANGILI NA MAJAMBAZI YAKAMATWA
KINACHOJIRI
KATIKA OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI, MAJANGILI NA MAJAMBAZI YAKAMATWA
WAKIWEMO WACHUUZI WA SMG KUTOKA BURUNDI, NG’OMBE ZATAIFISHWA, WAHAMIAJI HARAMU 425
WAMEKAMATWA WAKIWEMO WANAOWAHIFADHI.
Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo imetoa hukumu
ya kutaifisha Ng’ombe 103 mali ya Bw. Kalemela George kwa kosa la kuingiza
mifugo hiyo katika hifadhi ya taifa ya Biharamulo. Naibu Kamishna wa Polisi nchini Kamanda Simon
Sirro amewaambia waandishi wa Habari mjini Bukoba leo Jumatano Oktoba 2,2013
kuwa adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kifungu namba 111 cha sheria ya
wanayama pori na uhifadhi ya mwaka 2009.
Ng’ombe hao walikamatwa wakati Operesheni
Kimbunga awamu ya Pili inaendelea katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita
ambapo jumla ya Ng’ombe 2,220 walikamatwa kwenye hifadhi ya Taifa kwa kipindi
cha siku 10 tangu kuanza kwa awamu hii ya operesheni Septemba 21, 2013.
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, jumla ya
watuhumiwa 88 wa unyang’anyi wa kutumia silaha pamoja na silaha 23 zikiwemo
Bomu la kurushwa kwa mkono Moja, bunduki aina ya SMG 3, Pisto 2, Magobole18 na
Risasi 484 miongoni mwake zipo risasi za SMG/SAR 471 na risasi za Pisto 13,
magazine za SMG 2 na Sare za Jeshi la Burundi zimekamatwa katika kipindi cha
siku 10 za operesheni Kimbunga Awamu ya Pili.
Akifafanua, Kamanda Sirro amesema watuhumiwa
wawili wa ujambazi wa kutumia silaha wamekiri kufanya uchuuzi wa kununua silaha
nchini Burundi hususan silaha za Kivita za SMG na kuziuza nchini kwa Majambazi
wa kutumia Silaha.
Kamanda Sirro amesema mtu huyo bila kumtaja
jina ameiambia polisi kuwa awali alikuwa mfanyabiashara ya Mbuzi kutokea
Tanzania kwenda Burundi ndipo alipogundua biashara yake hiyo hailipi na kuamua
kujiingiza kwenye biashara ya kununua Bunduki aina ya SMG kwa shilingi
500,000/= kutoka Burundi na kuja kuziuza Tanzania kwa zaidi ya shilingi milioni
moja.
“Mtu huyu amekiri kuuza silaha nyingi nchini
ambazo amekuwa akiziingiza kutoka nchini Burundi. Serikali itazungumza na
Serikaliya Burundi kuona namna ya kudhibiti tatizo hilo nchini Burundi ambapo
silaha za SMG zisizotakiwa kumilikiwa na Raia isipokuwa Jeshi pekee
zinapatikana kirahisi,” alisema Kamanda Sirro.
Aidha, Majangili 11 wamekamatwa pamoja na meno
ya Kiboko na Ngozi ya Mbwea. Jumla ya
Makokoro 12, Bangi kilo Tatu, Gongo Lita271 na Magunia ya Mkaa 100
yaliyotengenezwa kwa mazao ya misitu kinyume na Sheria vimekamatwa katika mikoa
ya Kagera, Kigoma na Geita.
Wakati huo huo, Kamanda Sirro amesema katika
kipindi cha Operesheni Kimbunga Awamu ya Pili jumla ya Wahamiaji Haramu 425
walikamata wakiwemo watu 5 wanao tuhumiwa kwa kosa la kuwahifadhi na
kuwatorosha wahamiaji haramu. Miongoni mwa wahamiaji haramu waliokamatwa ni
Warundi 180, Wanyarwanda 149, Waganda 82 na Wakongo 14. Mkoa ambao unaongoza
kwa kukamata wahamiaji haramu wengi ni Kagera (209), Kigoma (166) na Geita (50).
Kamanda Sirro amesema operesheni Kimbunga
inaendeleza na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kuwabaini
wahalifu. “Ulinzi na Usalama wa nchi hii ni wetu wote,
tu shirikiane kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu na hasa ujambazi,
ujangili, uhamiaji haramu pamoja na haribifu wa mazingira” amesisitiza kamanda
Sirro.
Amesema Operesheni Kimbunga inaendelea kwa
kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi pamoja na kufuata Haki za Binaadam.
Wanaoshughulikiwa kwa kukamatwa na kuhojiwa ni watu wote wanaotiliwa shaka na
wanaobainika wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kurudishwa nchini kwao.
“
Katika utekelezaji wa operesheni hi mwananchi mwenye taarifa aonyeshe dhamira
ya kijasiri, kizalendo na mshikamano wa kitaifa katika kusaidia vyombo vya dola
kwa kutoa taarifa ili kukabili wahalifu na uhalifu nchini” alisisitiza Kamanda
Sirro.
Taari fa hii imeandaliwa na kusambaza na Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Bukoba, Oktoba2, 2013.
No comments:
Post a Comment