HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO KWA SERIKALI YA RAIS KIKWETE.
Ndugu wana
habari,napenda kuchukua nafasi hii kama Rais wa serikali ya wanafunzi chuo
kikuu katoliki cha sayansi ya Afya na Tiba(CUHAS-Bugando) kwa niaba ya
wanazuoni wote wa chuo hiki na kwa niaba ya wanafunzi wa sekta ya Afya wa vyuo
vikuu vyote visivyokua vya umma nchini(yaani vyuo vikuu vikuu vyote vya fani ya
afya vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na mashirika ya watu binafsi).Kuweza
kueleza kilio chetu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo
mbalimbali vya kiserikali vyenye mamlaka ya kusimamia Elimu ya juu na vyuo
vikuu nchini.
I:DHANA YA ASILIMIA MIA MOJA YA MKOPO.Watanzania
wengi wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu
wanaotugharamikia katika masomo yetu wanaelewa kwamba mwanafunzi anayesoma fani
za Afya kama Udakatari,Ufamasia,Uuguzi na nyinginezo kama hizo analipiwa kila
kitu na serikali kupitia bodi ya mikopo kwa hiyo hahitaji msaada wowote wa
kifedha kutoka kwa wazazi au walezi kwa kua anjitosheleza kwa kila kitu.Dhana
ambayo kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu kisichokua cha Umma ni
tofauti kabisa.Kwa kua asilimia mia moja inayoongelewa ni kama asilimia hamsini
tu ya karo zinazotozwa katika vyuo hivi.
Wanafunzi wote wa vyuo hivi vya fani ya
Afya visivyokua vya umma tumekua tukipokea kiasi cha shilingi za kitanzania
milioni mbili na laki sita tu(Tsh.2,600,000/=)
toka bodi ya mikopo kama mkopo kwa ajili ya Ada.Kiwango hiki kipo hivo
toka wakati huo ambapo katika vyuo hivi Ada ilikua inatozwa kwa kiwango hicho.Ni
takribani miaka sita sasa kiwango hiki kimebakia kama kilivo bila
kuongezeka.Wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa taasisi
hizi.
Ada zimekua zikiongezeka mwaka hadi mwaka na sasa kufikia takribani
milioni nne,na zaidi kama karo katika vyuo hivi mbalimbali Ikiwa ina maana
kwamba kiasi kinachobaki baada ya Tsh.2,600,000/= kutolewa kama mkopo
mwanafunzi mwenyewe inatakiwa ajilipie pamoja na gharama zingine ambazo si
sehemu ya karo zinazohitajika kutolewa.Wanafunzi wengi katika vyuo hivi
wanasoma na kuishi katika mazingira magumu sana kwa kua gharama anazotakiwa
kuchangia binafsi ni kubwa kiasi cha kuwalemea wanafunzi wengi ambao wengi wetu
ni watoto wa wakulima ila tukiwa na haki ya kupata Elimu bila kujalisha hali ya
uchumi wa familia zetu
.CHANGAMOTO;hali
hii imepelekea wanafunzi wengi wanaochaguliwa kushindwa kujiunga na vyuo hivi kwa
kushindwa kumudu gharama hizi,lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kupoteza
mda wao mwingi katika kufanya vibarua ili kupata kiasi cha kumalizia ada ambayo
imepelekea ufaulu wao kushuka na wengine kupoteza kabisa nafasi ya kuendelea na
masomo.
OMBI LETU KWA SERIKALI;kwa
kua tumejiunga na vyuo hivi kwa mfumo halali wa Tume ya vikuu Tanzania(TCU)
ambao haukuangalia hali ya kiuchumi ya familia zetu kama tutamudu au hatutamudu
kulipa gharama hizi,kwa kua tulijiunga na vyuo hivi kwani tulikua na vigezo vya
kusoma fani hizi kama wenzetu wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma na hata
zaidi na kwa kua tukihitimu sisi wote yaani wenzetu wanaosoma vyuo vikuu vya
umma na sisi tunaosoma vyuo vikuu visivyokua vya umma tunakwenda kuhudumia na
kuokoa uhai wa watanzania walewale.
Tunaiomba serikali iongeze kiwango hiki
tunachopewa kama mkopo kwa ajili ya ada,ili hiyo Asilimia mia moja inayosemwa
iwe na maana kwetu kwa kua kwa sasa ni kama nusu tu.Wengi wanashindwa kujiunga
na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizo.Katika nchi yenye upungufu wa
60% ya madaktari na wataalamu afya kwa ujumla,pia katika nchi ambayo daktari
mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 33 elfu.Si vema kuona vijana wenye dhamira
na nia thabiti ya kuokoa maisha ya watanzania wanashindwa kutimiza ndoto hizo
za kua wataalamu wa Afya ati kwa kushindwa kulipa karo.
Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU):Upandishwaji
Ada katika vyuo vikuu visivyokua vya umma usiofuata utaratibu na Kile
kinchojulikana kama “List of Approved programme fees” ikiainisha gharama za ada
zinazotozwa katika vyuo vikuu vyote nchini.Tume vya vikuu Tanzania imepewa
mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya vikuu No.7,2005.Kusimamia kuanzia
udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu vyote nchini vya umma na visivyokua vya
umma.Central Admission system
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII;Institute of Health and Allied Health
sciences.
Kumekuwa na changamoto kubwa
katika gharama za ada, chakula na makazi kwa wanafunzi wa stashahada katika
vyuo vya Afya hasa vile vya binafsi ambapo gharama za uchangiaji zinazidi kuwa
kubwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao hutejigemea kiasi kikubwa na kuwa
serikali kupitia wizara ya afya imekua ikitoa fedha kwa ajiri ya wanafunzi hao.
OMBI LETU:-Tunaiomba Serikali kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka wazi ni kiasi gani inachangia kwa kila
mwanafunzi mmojammoja wa stashada katika vyuo vya afya kwa kueleza mchanganuo
halisi ili kuwawezesha wanafunzi hao kutambua ni kwa kiasi gani Serikali
kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii inachangia kama ulivyo utaratibu wa
bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa shahada .
Vilevile kumekuwa na changamoto ya mabadiliko
ya gharama za ada kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya na
kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi hao hivyo Tunaiomba Serikali kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kutoa gharama halisi ambazo wanafunzi wa
stashada katika vyuo vya Afya watapaswa kuchangia katika vyuo mbalimbali
ikiwemo vile vya binafsi.
Kulingana na changamoto
mbalimbali zinazozidi kujitokeza kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya
afya, Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
Kuboresha mfumo wa uwezeshaji kwa
wanafunzi wa stashada na kuweka mfumo na taratibu zitakazosimamia mabadiliko ya
ada katika vyuo mbalimbali vya Afya ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali
zinazojitokeza vyuoni hasa vya binafsi.
Kumekuwa na uchakavu wa
miundombinu inayomilikiwa na wizara ya Afya katika vyuo vya afya na hivyo
kupunguza ufanisi wa masomo kwa wanafunzi hivyo Tunaiomba Serikali kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha miundombinu mbalimbali
inayomilikiwa na wizara ya afya katika vyuo vya Afya vinavyotoa stashahada.
No comments:
Post a Comment