TAMASHA LA SANAA LA JAMBO FESTIVAL KUKUTANISHA WASHIRIKI ZAIDI YA 100 NDANI NA NJE YA NCHI.
ZAIDI ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki
kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba
23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa.
Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo
Festival 2013 ,Augustine Namfua alisema kuwa , tamasha hilo ni la pili
kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni
kuwawezesha washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za
kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa, tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha
washiriki kutoka nchi za Ufaransa,na Angentina ambao wataweza kuonyesha
matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za
kitamaduni .
Alisema kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili
ikiwemo maonyesho ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili
kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha, na Dar es Saalamu .
Namfua aliongeza kuwa, pia
kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa pamoja na onyesho
la mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo katika tamasha hilo kwa
siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo yatakuwa yakionyeshwa
.
Aliongeza kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu
mbalimbali wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na
maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kushiriki katika tamasha hilo .
‘tamasha la mwaka jana lilifana sana
kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na
lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya
kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa
wenzetu wan je ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi
hivyo tunatarajia watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha
hilo’alisema Namfua.
Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika
katika tamasha hilo na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni
zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za kiafrika , huku
akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo katika kusaidia matamasha
hayo ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment