OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFUNGUA OFISI 23 MIKOANI
4793 Wakili wa serikali Mkuu, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Frederick Manyanda (kulia) akieleza kwa waandishi
wa (hawapo pichani) mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma
ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu kwa kufungua
ofisi zaidi Mikoani, Katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Habari toka ofisi
hiyo Bi. Asiatu Msuya na Kulia kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi.
Georgina Misama.
4793 Wakili wa serikali Mkuu, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Frederick Manyanda (kulia) akieleza kwa waandishi
wa (hawapo pichani) mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma
ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu kwa kufungua
ofisi zaidi Mikoani, Katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Habari toka ofisi
hiyo Bi. Asiatu Msuya na Kulia kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi.
Georgina Misama.
========= ===== ====
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
OFISI
YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFUNGUA OFISI 23 KATIKA MIKOA
MBALIMBALI KUFANIKISHA MPANGO WA UTENGANISHWAJI WA SHUGHULI ZA UPELELEZI
NA UENDESHAJI WA MASHTAKA NCHINI
______________________________
Utangulizi
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanikiwa kufungua Ofisi 23 katika mikoa ya
Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro (Moshi), Arusha, Mwanza,
Kagera (Bukoba) Mara (Musoma), Shinyanga, Tabora, Singida, Iringa,
Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, Rukwa (Sumbawanga),Ruvuma (Songea),
Njombe, Manyara,Morogoro,Kigoma,Geita na Pwani. Aidha jumla ya Ofisi
mbili (2) za zimefunguliwa katika Wilaya za Temeke na Monduli. Kwa
mwaka wa fedha 2012/2013 pekee jumla ya Ofisi tano (5) zimefunguliwa
katika mikoa ya Pwani, Kigoma, Morogoro, Manyara, Njombe na Geita
ikiwemo pia Ofisi mbili za Wilaya.
Lengo
Lengo kuanzishwa
na kuimarishwa kwa Ofisi hizi za Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha kuwa
huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa
karibu zaidi. Baadhi ya huduma zinazotolewa ni pamoja na kuendesha
Mashtaka mahakamani, kushughulikia malalamiko na kero za wananchi
kuhusiana na kesi za jinai na madai zinazowakabili, kutembelea mahabusu
na kuratibu upelelezi wa kazi za upelelezi wa makosa ya jinai
zinazofanywa na vyombo pelelezi/chunguzi ikiwemo Polisi, Magereza,
Uhamiaji,TAKUKURU.
Utekelezaji wa Mpango wa kutenganisha Upelelezi na Mashtaka nchini
Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kutekeleza mpango huu wa Utenganishwaji wa Upelelezi na Mashtaka kwa mujibu wa Sheria ambapo mfumo wa Sheria ambao uliwezesha kutungwa kwa Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, 2005 na Sheria ya Usimamizi wa Uendeshaji Mashtaka nchini, 2008 umeboreshwa; pamoja na kuanzishwa
kwa Jukwaa la Ki-taifa la Haki-Jinai (National Criminal Justice Forum)
Desemba 2009 linaloviunganisha pamoja vyombo vyote vinavyosimamia
utolewaji wa Haki-Jinai nchini;
Serikali
pia imeboresha Muundo wa Divisheni ya Mashtaka kwa kuweka Sehemu
(Section) mahsusi inayosimamia utekelezaji wa mchakato wa utenganishaji
wa kazi za upelelezi na Mashtaka na uratibu wa kazi za ki-pelelezi;
pamoja na kuanzishwa kwa huduma ya Mashtaka ya moja kwa moja ambako
Mawakili wa Serikali wanaendesha kesi; Hii imepelekea idadi ya kesi
zinazofunguliwa Mahakamani ambako Mawakili wa Serikali wanaendesha
Mashtaka kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma; Kuongezeka kwa
ubora wa huduma zitolewazo na kupungua kwa kesi za kubambikizwa.
Utekelezaji
wa Programu ya Utenganishwaji wa Mashtaka na Upelelezi
(Civilianization) imetoa msukumo mkubwa kwa Ofisi kuingia uanachama na
makubaliano ya mashirikiano na vyama vinavyohusiana na kazi za
Uendeshaji Mashtaka duniani, kama vile-IAP, HOPAC, APA, EAAP, na
ARINSA; Serikali itaendelea kupanua wigo wa
uendeshaji wa Mashtaka kwa kuanzisha na kuimarisha Ofisi katika Wilaya
zote nchini pamoja na Mikoa miwili iliyobaki ya Katavi na Simiyu.
Tunapenda
kuwakumbusha Wadau wetu wote na Wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa
mbele katika kutoa taarifa za uhalifu au jinai yoyote katika jamii kwa
vyombo husika kupitia utaratibu unaofaa; na kutoa ushahidi Mahakamani
pale unapohitajika kwa kuwa hizi ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa
kesi mbalimbali. Aidha tunatoa wito kwa umma, wadau wetu na wananchi
wote kwa ujumla pamoja na vyombo vya habari nchini kufuatilia mtiririko,
hoja zinazowalishwa Mahakamani na uamuzi uliotolewa na Mahakama katika
kesi mbalimbali zinazoendelea kuwa na taarifa sahihi ya kuhusu kesi
hizo.
Imetolewa Na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ijumaa, Septemba 27, 2013
Kwa mawasiliano zaidi
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
SLP 9050
KIVUKONI FRONT
DAR ES SALAAM
SIMU: +255 22 21181778
NUKUSHI: +255 22 2113236
BARUA PEPE: info@agctz.go.tz
TOVUTI: www.agctz.go.tz
No comments:
Post a Comment