Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni.
Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr Khalfany Haule
Na Mwandishi Wetu, Handeni
SERIKALI
kwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr
Khalfany Haule, imebariki kufanyika kwa tamasha la utamaduni la Handeni
Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani humo.
Tamasha
hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la
kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango
wenye mashiko kwa sekta hiyo.
Akizungumza
juzi mjini hapa, Dr Haule alisema ni kitendo kinachopaswa kuungwa mkono
na serikali yote ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kupitia njia
mbalimbali.
Alisema
wao kama wilaya wamepokea kwa mikono miwili wazo zuri la kuandaliwa kwa
tamasha hilo wilayani Handeni mkoani Tanga, hivyo watakuwa pamoja na
waandaaji.
“Tunashukuru
kwa dhati kuona mwaka huu mwishoni kunafanyika tamasha hili lenye mguso
wa aina yake, maana watu watakutana kuangalia mambo ya utamaduni wa
Handeni na Tanzania kwa ujumla.
“Tupo
tayari kushirikiana kwa karibu na waandaaji wa tamasha hili ili
lifanyike kwa mafanikio na kuleta ari mpya katika sekta ya maendeleo ya
Taifa, hususan wilayani Handeni,” alisema Haule.
Tamasha
la Utamaduni wa Handeni linafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuandaliwa
na Raha Company And Entertainment likiwa na malengo ya kukuza na
kutangaza sekta ya utamaduni na utalii hapa nchini na kusubiriwa kwa
hamu wilayani humo.
No comments:
Post a Comment