Katiba ni Mwafaka wa Kitaifa. Viongozi zungumzeni.
Na Zitto Kabwe
Kwa
takribani wiki tatu sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu muswada wa
sheria uliopitishwa na Bunge ili kufanya marekebisho ya sheria ya
marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011. Mjadala na upitishaji wa sheria hii
uliweka rekodi ya pekee katika nchi yetu kwa vitendo vya kihuni kutokea
Bungeni ambavyo nisingependa kuvirejea kutokana na aibu kubwa ambayo
Bunge liliingia.
Kiukweli
kuna sintofahamu katika nchi kuhusu kuandikwa kwa Katiba mpya. Hii
imechangiwa na kurushiana maneno miongoni mwa wanasiasa wa pande zote
mbili, wanaopinga muswada ulivyo na wanaounga mkono muswada ulivyo.
Masuala
ya Tume imalize kazi yake lini, ushiriki wa Zanzibar na idadi ya
wajumbe kutoka Zanzibar kwenye Bunge la Katiba, Wajumbe wa Bunge Maalumu
wanapatikanaje na kadhalika ni masuala ambayo yanaweza kupatiwa mwafaka
kwa viongozi kukaa na kuzungumza.
Haya
sio masuala ya kushindwa kujenga mwafaka labda kuwe na nia mbaya dhidi
ya mchakato wa kuandika Katiba mpya. Katiba sio suala la kufanyia siasa.
Katiba ni uhai wa Taifa.
No comments:
Post a Comment