OFISI YA TTB KANDA YA ZIWA MWANZA YAZINDULIWA RASMI NAIBU WAZIRI, ASEMA TATIZO LA BAJETI FINYU KWA TTB LITAPATIWA UFUMBUZI
Ofisi
ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kanda ya ziwa iliyoko katika jingo la
hotel ya Mwanza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB). Kikundi
changoma kutoka kituo cha utamaduni cha Bujora mkoani Mwanza kikitoa
Burudani ya ngoma ya kucheza na chatu mbele ya ofisi ya Bodi ya Utalii
kanda ya ziwa jijini Mwanza mara ru baadaya mgeni rasmi Naibu Waziri
Lazaro Nyalandu kuwasili ofisini hapo ili kuizindua ofisi hiyo. Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazro Nyalandu (MB) akizungumza na
wandishi wa habari ndani ya ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kanda
ya ziwa jijini Mwanza muda mfupi baadaya kuizindua . Kushoto ni
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki.
……………………………………………………….
Na Geofrey Tengeneza, Mwanza
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB) ameiambia ya
Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kuwa tatizo la sugu bajeti isiyotosheleza
mahitaji ya Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake litapatiwa
ufumbuzi kwa kiasi kikubwa mara baada ya fedha kwa ajili ya mfuko wa
maendeleo ya Utalii (Tourism Development Levy kuanza) kuanza rasmi
ambapo moja ya vyanzo vyake vya fedha ni tozo la kitanda siku kwa
watalii watakaokuwa wakilala katika hoteli mbalimbali.
Mheshimiwa
Nyalandu ameyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Bodi ya Utalii kanda
ya ziwa iliyoko jijini Mwanza. Amesema Bodi ya Utalii inapaswa kutengewa
bajeti ya kutosha kuiwezesha kumudu ushindani uliopo wa kutangaza
vivutio vyetu katika masoko ya watalii na kuvutia watalii wengi. “
Tuiwezeshe kwanza TTB kwa kuipa fedha za kutosha kutekeleza majukumu
yake ndipo tuwaluamu wakishindwa” alisema. Kuzinduliwa kwa ofisi ya TTB
mkoani Mwanza ambako kumefanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya
Utalii duniani ni jitihada za Bodi ya Utalii Tanzania kusogeza huduma
zake zaidi kwa wananchi ambapo ofisi hii ya Mwanza ni ya tatu, baada ile
ya Kanda ya Kaskazini na ile ya Kanda ya nyanda za juu Kusini iliyoko
mjini Iringa. Ofisi hii ilianza kazi jijini Mwanza tangu Novemba 11,
2011 ambapo awali ilianzia katika eneo la Kapripointi kabla ya kuhamia
katika jengo la hoteli ya Mwanza (Mwanza Hotel) katikati ya jiji hili la
Mwanza Desemba 27, 2012.
Tangu
kufunguliwa na kuanza kutoa huduma mkoani Mwanza ofisi hii ya bodi ya
Utalii imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi
ya wageni hususan wa nje wanaotembele ofisi hii ili kupata taarifa ya
vivutio vya utalii vilivyopo hapa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla.
Kwa mfano kuanzia Desemba 26, 2012 hadi Machi 2013 idadi ya wageni
waliotembelea ofisi yetu walikuwa 102; kuanzia Aprili hadi June 2013
walikuwa 97; na kuanzia Julai hadi tarehe 27/9/2013 ofisi hii
ilopozinduliwa rasmi idadi ya wageni imefikia 242. Hivyo jumla ya wageni
(watalii) kutoka nje ya nchi waliotembelea na kupata taarifa za utalii
katika ofisi yetu toka imefunguliwa ni 441.
Mafanikio
mengine ni pamoja na Bodi ya Utalii kupitia kitengo chake cha Utalii wa
Utamaduni (Cultural Tourism Program) kwa kushirikiana na ofisi hii ya
Kanda kuanza kutoa huduma za ushauri wa kuendesha kuiutaalamu zaidi
shughuli za Kikundi cha Utalii wa Kitamaduni cha Kisesa (Kisesa Eco
& Cultural Tourism). Tunatambua na kushirikiana na Kituo cha
Kumbukumbu cha Kabila la Wasukuma cha Bujora na ambacho tumekuwa
tukikitangaza kwa muda mrefu sasa kama moja ya vivutio vilivyoko hapa
Mwanza. Aidha ofisi yetu hii ya Kanda hapa Mwanza mpaka sasa imeweza
kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi sita kutoka vyuo
mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-SAUT. Aidha
kupitia ofisi ya Kanda Bodi ya Utalii Mwezi Februari ilileta mkoani
Mwanza wandishi wa habari wa kimataifa wawili kutoka Uturuki ili
kuandika na kupiga picha vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Mwanza kwa
lengo la kuvitangaza katika nchi hiyo
Kufunguliwa
kwa ofisi hii ya Kanda kutasaidia kwa kiasi kikubwa sana katika
kuvitangaza vivutio vya utalii vya hapa Mwanza na Kanda ya ziwa na
itakuwa ni chachu ya maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na
katika Kanda ya ziwa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment