Jumuiya ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate
Jumuiya
ya waKenya DMV waomboleza mauwaji ya Westgate, Siku nane tangu kutokea
kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua zaidi ya watu 67 na
kujeruhi wasiopungua 175.
MC
Humphrey OneMic Muturi akiwa Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial
Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya kuomboleza mauwaji ya Westgate.
Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)
Wakenya kutoka sehemu mbalimbali duniani wameungana na wenzao katika maombi na ishara za matumaini kwa wenzao wa nchini Kenya.
Baadhi
ya waKenya kutoka sehemu mbalimbali hapa DMV Siku ya Jumapili Sept 29
walikutana Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini
Washington, D.C kwa maombolezo ya mauwaji yaliotokea jijini Nairobi siku
ya Jumamosi Sept 29 ndani ya Westgate Mall jijini Nairobi Kenya.
Pastor Maurice Kinyanjui akifungua hafla hiyo kwa dua maalumu ya maobolezo ya mauwaji ya Westgate yaliofanyika Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C
Jumuiya
ya waKenya na rafiki wa wanajumuia hao walikutana Mbele ya mjengo wa
Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya
kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapa matumaini wenzao walioathirika na tukio
hilo.
Walianza
kwa ufunguzi kuwaombea dua walioathirika na tukeo hilo lilitokea Siku
ya Jumamosi Sept 21, ambapo kundi la Al shabab walivamia na kuteka eneo
la sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate Mall Jijini Nairobi
Kenya.
Siyad Warsame Ali akisoma dua maalumu ya maobolezo ya mauwaji ya Westgate yaliofanyika Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C Waliendelea
kwa kukumbushana mengi yakiwemo kusisitiza kwa upendo wa kua kitu
kimoja bila ya kujali tafauti zao na kuvumilia kwa yote yaliotokea kwani
Kenya ni nchi ya amani.
Siku nane tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi nchini Kenya, lililoua
zaidi ya watu 67 na kujeruhi wasiopungua 175.
Wanajumuiya
ya waKenya waliohudhuria katika hafla ya maombolezo ya mauwaji ya
Westgate wakiwa na watoto waliobeba bendera za taifa, Siku ya Jumamosi
Sept 21, Mbele ya mjengo wa Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C.Wakenya kutoka sehemu mbalimbali duniani wameungana na wenzao katika maombi na ishara za matumaini kwa wenzao wa nchini Kenya. Jumuiya
ya waKenya na rafiki wa wanajumuia hao walikutana Mbele ya mjengo wa
Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C., kwa ajili ya
kuwakumbuka, kuwaombea na kuwapa matumaini wenzao walioathirika na tukio
hilo.
Baadhi
ya waKenya wakimakinika kwa huzuni ya maombolezi ya kuwakumbuga ndugu
jamaa na marafiki waleopoteza maisha katika shambulio lilofanywa Siku ya
Jumamosi 21, na wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya Westgate Mall
nchini Kenya.
Walianza
kwa ufunguzi kuwaombea dua walioathirika na tukeo hilo lilitokea Siku
ya Jumamosi Sept 21, ambapo kundi la Al shabab walivamia na kuteka eneo
la sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate Mall Jijini Nairobi
Kenya.
Waliendelea
kwa kukumbushana mengi yakiwemo kusisitiza kwa upendo wa kua kitu
kimoja bila ya kujali tafauti zao na kuvumilia kwa yote yaliotokea kwani
Kenya ni nchi ya amani.
Wanajumuiya ya waKenya DMV aliposhikilia mishuma kwaajili ya kuomboleza mauwaji ya Westgate
Baada
ya hapo waliimba wimbo wa taifa wa Kenya na kuwasha Mishumaa kama ishara
ya matumaini na upendo juu ya kuombolza tokeo hilo ambalo lilikua
chukizo kwa dunia nzima, na baadhi ya wageni mbali mbali waliotembelea
Abraham Lincoln Memorial Jijini Washington, D.C waliwaunga mkono dhidi
ya kitembo cha haramu kilichofanywa na kundi la kigaidi la Alshabab.
Baadhi ya wakenya kutoka sehemu mbalimbali DMV wakiwasha mishumaa kwa kuomboleza.
No comments:
Post a Comment