Amiri Jeshi mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili katika Uwanja wa Uhuri akiwa kwenye gari maalum la Kijeshi na
Sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis
Mwamunyange walipokuwa wakioa salamu kwa wananchi na wageni mbali mbali
waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa
Tanzania Bara.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,
Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho Miaka 51 ya
Uhuru wa Tanzania Bara,leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja
na viongozi wengine wa Serikali wakipokea salamu za heshima kutoka kwa
Vikosi mbali mbali vya Ulinzi la Usalama wakati wa maadhimisho ya miaka
51 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika
maadhimisha hayo,kutoka kulia ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo,Mh. Joseph Kabila,Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji,Mh.
Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt.
Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mzee Ali Hassan
Mwinyi.
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib
Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani
hapo.katikati ni Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha wanaanga cha Jeshi la
wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi
Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Kikosi cha ardhini Jeshi la
wananchi la Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi
Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama
vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri
jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete.Picha na Full Shangwe Blog.
No comments:
Post a Comment