MBUNGE WA WAWI ALIYEFIWA NA MKEWAKE JANA USIKU AFIKWA NA JANGA JINGINE MCHANA HUU!
PAMOJA na kufikwa na msiba wa kufiwa na mkewake mdogo jana usiku Mbunge
wa Wawi Hamadi Rasid Mohamed, leo hii amefikwa na tukio jingine la
kuangushwa kwenye kesiyake yake na wenzake dhi ya Chama cha Wananchi
CUF. Kwa mujibu wa taarifa zilizo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na
Naibu katibu Mkuuwa chama Cha Wananchi CUF Tanzania bara Julius Mtatiro
maamuzi hayo yametolewa mchana huu Mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar
es Salaam. Taarifa kamili ya naibu katibu mkuu huyo ni hii hapa;
Hii ina maana kwamba OMBI la Hamad Rashid na mawakili wake kuwa WAJUMBE WOTE WA BARAZA KUU la CUF wafungwe jela kwa kukiuka amri ya mahakama limetupiliwa mbali.
Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013 ambapo mawakili wa chama watapangiwa tarehe YA kuleta hoja za kutaka kesi ya msingi ifutwe kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na walifukuzwa kihalali na kwa kuzingatia katiba ya chama.
Chama chetu kimefurahishwa na uamuzi huu kwani unaonesha namna ambavyo hatukukurupuka. Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki. Chanzo; Raha za Pwani Blo
TUMESHINDA KESI YA AWALI AMBAYO MHE.
HAMAD RASHID NA WENZIE WALIKISHTAKI CHAMA.
Hukumu imemalizika muda so mrefu hapa
mahakama kuu.
Hoja zote za akina Hamad Rashid
zimetupiliwa mbali.
Mahakama imejiridhisha kwamba, amri ya
mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR na
wenzake wanne haikufikishwa kwa chama kwa hivyo kikao husika kilikuwa halali.
Hii ina maana kwamba OMBI la Hamad Rashid na mawakili wake kuwa WAJUMBE WOTE WA BARAZA KUU la CUF wafungwe jela kwa kukiuka amri ya mahakama limetupiliwa mbali.
Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013 ambapo mawakili wa chama watapangiwa tarehe YA kuleta hoja za kutaka kesi ya msingi ifutwe kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na walifukuzwa kihalali na kwa kuzingatia katiba ya chama.
Chama chetu kimefurahishwa na uamuzi huu kwani unaonesha namna ambavyo hatukukurupuka. Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki. Chanzo; Raha za Pwani Blo
No comments:
Post a Comment