Prime time promotions ltd yatoa msaada wa vyakula kituo cha watoto yatima cha Mwana Orphan Centre jijini dar
Pichani shoto ni Mlezi wa kituo cha
kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu kiitwacho Mwana Orphan
Center kilichopo Vigunguti,jijini Dar Es salaam,Mama Ummy akitoa mkono
wa shukurani kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions
Ltd.Juhayna Ajmi Kusaga (pichani kulia),mara baada ya kuwapelekea msaada
wa vyakula mbalimbali.
Baadhi ya watoto wa kituo hicho
wakisaidiana kubeba baadhi ya misaada ya vyakula iliyotolewa na Kampuni
ya Prime Time Promotions Ltd.
Uongozi wa Prime Time Promotions
ukioneshwa sehemu ambayo baadhi ya watoto wa kituo hicho hulala wakati
wa usiku,kama uonavyo pichani,Watoto hao hulala sehemu hiyo ya wazi
kutokana na ukweli kwamba kituo hicho kimelemewa na watoto,kituo hicho
mpaka sasa kina idadi ya watoto wapatao 6o, na eneo halitoshi,kutokana
na hali hiyo kituo hicho bado kinahitaji msaada mkubwa wa mambo
mbalimbali ikiwemo kuwapatia sehemu nyingine nzuri ya kulala watoto hao.
Pichani kati ni Mlezi wa kituo cha
kulelea Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kiitwacho Mwana
Orphan Center kilichopo Vigunguti,jijini Dar Es salaam,Mama Ummy
akielezea hali halisi ya kituo hicho kilivyoanza na kinavyojiendesha
mpaka hivi sasa mbele ya Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions
Ltd.Juhayna Ajmi Kusaga pichani kulia na shoto ni Meneja Mipango wa
kampuni hiyo ya Prime Time,Balozi Kindamba.
Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time
Promotions Ltd.Juhayna Ajmi Kusaga pamoja na Mama Mlezi wa kituo hicho
wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho cha Mwana
Orphan Center.
Kwa mtu yeyote kwa mawasiliano na kwa msaada wowote.







No comments:
Post a Comment