KATIBU CCM, NORTH LONDON AGOMBEA NEC,UWT, TAIFA
Mkuu
wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma (kulia)
akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya NEC na Uwakilishi wa UWT Taifa,
Neema Kumba.
Neema Kumba.
Na Andrew Chale
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa (UVCCM) na Msomi wa digrii
ya uchumi, Neema Kumba amejitosa kwenye uchaguzi mkuu wa umoja huo
Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na uwakilishi UWT.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, muda mfupi baada ya
kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM,
Taifa, Sophia Duma,
Kumba
ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini
Uingereza,alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni
kuakikisha mikakati thabiti inajengeka kwa kiwango kikubwa miongoni mwa vjana na wanawake wote nchini.
“Kwa
umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu
ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia
wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua
wakisahauriwa na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.
Mbali
na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari
alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.
Mpaka
sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua fomu
za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.
No comments:
Post a Comment