Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Mh Leonidas Gama
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha
walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni
hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo
mjini Moshi jioni hii.
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili
mjini Moshi jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi
ya siku tatu.
Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa
Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na
matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha
safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro
Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo itakayofanyika kesho
Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya
Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua
Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika
kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais
Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati
wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Imetolewa na
KURUGENZI
YA MAWASILINO YA RAIS
MARCH 4, 2012
MOSHI
No comments:
Post a Comment