Na
Mwandishi WetuMASHABIKI
watakaofika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kushuhudia onesho
la tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 8 mwaka huu,
watalazimika kulipa kiingilio kidogo cha sh. 2,000 na sh. 5,000 kwa
viti vya kawaida.Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama wa Kampuni ya
Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa wametenga viingilio
katika kategoria tatu tofauti.Msama alisema watoto watalipa sh. 2,000, mashabiki watakaokaa
viti maalumu watalipa sh. 10,000 na watakaokaa viti vya kawaida
watalipa sh. 5,000, na tiketi za kategoria zote hizo zitauzwa
mlangoni. Alisema tiketi za
viti maalumu watakaohitaji wanaweza kupiga simu selula 0713 383838,
0786 383838 na 0786 373737 ili kupata tiketi na maelezo kinagaubaga.
"Tumeamua kuweka kiingilio kidogo
cha wastani ili kila mmoja apate fursa ya kushuhudia tamasha la
Pasaka wakiwamo watoto," alisema Msama. Msama alisisitiza kuwa tamasha hilo
litahudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema tamasha hilo lina lengo
la kuchangia watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa
ukimwi na mitaji ya wanawake wajane wasiojiweza. Fedha zilizopatikana katika tamasha la
mwaka jana zilitumika kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea
katika kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Gongo la Mboto, Dar
es Salaam na pia kuwapa mitaji wajane wasiojiweza. Baadhi ya wasanii wa nyimbo za Injili
waliothibitisha kupamba tamasha hilo mwaka huu ni Upendo Kilahiro,
Upendo Nkone, Atosha Kissava na kundi la Glorious Celebration.
Mbali na Dar es Salaam, tamasha la
Pasaka pia litafanyika mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja
wa Jamhuri ambayo ni Jumatatu ya Pasaka. Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia
litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika
ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.
No comments:
Post a Comment