
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Songea kupitia tiketi ya CCM
na Mjumbe wa bodi ya baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa
kazini kuendesha harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuboresha
miundombinu ya kituo cha Mafunzo na Utangazaji cha Mlimani TV jana.
Aliweza kuchangisha zaidi ya Milioni 30. Injinia Manyanya amezindua
harambee hiyo jana ambapo amewaomba wadau kuendelea kuchangia kwa
maendeleo ya habari nchini

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Yunus Mgaya akimkabidhi zawadi ya
ukumbusho (Wheel Cover ya Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano
ya Umma) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama shukurani
kwa ushirikiano wake katika kuendesha gurudumu la maendeleo ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Uandishi wa Habari
na Mawasiliano ya Umma Profesa Bernadikta Kilian na Meya wa Manispaa
ya Kionondoni Yusuf Mwenda.

Baadhi ya wafanyakazi na wadau wa taasisi
ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam wakitoa mchano wao, hapo wakiongozwa na Associate Dean Mr.
Irigo. Kulia akiwa muendesha harambee hiyo Injinia Stella Manyanya.

Baadhi ya wanafuni wa Undergraduate katika
taasisi hiyo wakitoa mchango wao wakiongozwa na Rais wao anaezungumza
kwenye Mic. Kulia akiwa muendesha harambee hiyo Injinia Stella Manyanya

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliaga
kwenye hafla hiyo kwa kulifungulia Rumba kama inavyoonekana pichani.
Wengine walioungana nae ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Profesa Yunus Mgaya, Mkuu wa Taasisi ya Uandishi wa Habari na
Mawasiliano ya Umma Profesa Bernadikta Kilian na Meya wa Manispaa ya
Kionondoni Yusuf Mwenda.

Baadhi ya wadau waliohudhuria
harambee hiyo wakifuatilia moja ya matukio katika hafla hiyo.Picha na Hamza Temba-Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Wa Rukwa
--
Na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Songea kupitia tiketi ya CCM
na Mjumbe wa bodi ya baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewaomba
wapenda maendeleo ya vyombo vya habari nchini ikiwepo Serikali,
Mashirika ya umma, Taasisi binafsi , Makampuni na watu binafsi
kuchangia kuboresha kituo cha Televisheni cha Mlimani TV
kinachomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa
Mkoa aliyasema hayo jana kwenye hafla ya kusherehekea mafanikio ya
vyombo vya habari vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuukaribisha
mwaka mpya 2012 wakati akizindua mpango endelevu kwa ajili kuchangia
kituo hicho (Fund Rising) uliyofanyika katika Taasisi ya Uandishi wa
Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IJMC) na
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vyombo vya habari
nchini.
Zaidi ya
shilingi milioni 30 zilipatikana jana ambapo fedha taslimu zilikuwa
alfu 50 na ahadi zikiwa zaidi ya milioni 30. Harambee hiyo iliongozwa na
Mhe. Manyanya ambaye binafsi alichangia shilingi milioni moja akiwa
kama mjumbe wa baraza kuu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mdau mkubwa
wa vyombo vya habari nchini.
Wengine waliochangia ni Naibu Makamu Mkuu
wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya ambaye alichangia shilingi Milioni
moja na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Bernadikta Kilian ambaye alichangia
shilingi laki sita. Wengine baadhi waliochangia ni walimu wa chuo
hicho, wanafunzi, Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Ilala, Home Shopping
Centre na Ubalozi wa Marekani waliochangia shilingi milioni 15.
Injinia Manyanya
alisema kuwa kuna haja kubwa ya kuboresha Studio ya Mlimani TV na
vyombo vyake vya kufundishia kutokana na umuhimu wa chuo hicho nchini
kwa ajili ya kuzalisha waandishi wa habari bora kwa kuzingatia misingi
ya taaluma. Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo taasisi pekee ya Umma inayotoa
mafunzo ya Uandishi wa habari nchini.
"Tuungane pamoja kuhakikisha vifaa
vinavyohitajika vinapatikana kwani leo hii tunazindua mkakati wa
kuchangia kuiwezesha taasisi hii iweze kuendesha shughuli zake kwa
kufuata ueledi wa tasnia ya vyombo vya habari nchini kwa kuzalisha pia
waandishi bora na sio bora waandishi. Hiyo ni kutokana na umuhimu wa
waandishi wa kwani wana uwezo mkubwa wa kutumia taaluma yao kuleta
amani au vurugu katika nchi" Alisema Injinia Manyanya.
Hapo kabla Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam kina Mpango mkakati wa miaka 50 ijayo ambapo lengo
lake kubwa ni kuimarisha miundombinu na kuboresha vipindi vya taaluma
ambapo alikiri kuwa zoezi hilo hawataweza kulifanya wenyewe jambo
lililowalazimu kuzindua mkakati huo wa kuchangisha fedha kwa ajili ya
kufikia malengo hayo.
No comments:
Post a Comment