MAASHIMISHO SIKU YA WANAWAKE WAKRISTO (WWK)
Mama Mchungaji Elizabeth Mboma (53) akionesha vazi la shule lenye staha ili kuwaonya mabinti wanaovaa sare za ajabu shuleni, wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Wakristo (WWK) katika Kanisa la TAG Mwenge jijini Dar es Salaam juzi, ambapo maonesho ya mavazi ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho hayo. Wengine ni wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Alpha wanaosali katika kanisa hilo. (NA MPIGAPICHA WETU)
Mchg. Tumaini Mwanyonga
akiangalia keki yenye umbo la Biblia mara baada ya kuzindua maonesho ya
bidhaa ya bidhaa za chama cha Wanawake Wakristo (WWK) wa Kanisa la TAG
Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
WWK Mwenge, Bi. Beatrice Simba akitoa maelezo kuhusu keki hiyo.
Wanawake Wakristo (WWK)
wa Kanisa la TAG Mwenge jijini Dar es Salaam wakiingia kanisani ili
kuanza ibada maalum ya kuadhimisha siku yao jana.
Mama Mchg. Patience
Mitimingi akiongoza wimbo maalum wakati wa kuadhimisha siku ya Wanawake
Wakristo (WWK) katika Kanisa la TAG Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Kulia ni Bi. Mariam Wanga akifurahia wimbo huo.
2
2
Akinamama wa TAG Mwenge
wakionesha mitindo ya mavazi ya jioni yenye staha ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya Wanawake Wakristo (WWK) katika Kanisa la TAG
Mwenge jijini Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA IRENE BWIRE





No comments:
Post a Comment