BREAKING NEWS:MASHUJAA YAIBOMOA TENA TWANGA , SASA HIVI NI LILIAN INTERNET
BENDI
ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imezidi kuibomoa bendi ya
African Stars ‘Twanga Pepeta’ baada ya kumyakua mnenguaji wake
mahiri,Lilian Tungaraza maarufu kama ‘Intanet’.
Meneja
wa Mashujaa Band Maximilian Luhanga alisema kwamba wamweamua kuwachukua
wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika idara hizo na tayari
wameshasaini mkataba wa kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili ambao
onyesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika jumatano ijayo katika
ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Hii
ni mara ya pili kwa Mashujaa kuibomoa Twanga Pepeta ambapo mapema mwaka
huu ilimyakua mmmoja ya waimbaji mahiri, Charlz Gabriel ‘Chaz
Baba’..Kwa hisani ya Mama Pipilo Blog

No comments:
Post a Comment