WATU WAWILI WAHOFIWA KUFA VURUGU ZA SONGEA
Kuna
raia wanauawa tangu juzi na matukio yanaripotiwa ila askari hawachukui
hatua yeyote ile zaidi wanasema ushahidi hawajauona,usiku wa kuamkia
leo limekua tukia la 5 raia kuuliwa na askari kama kawaida yao hawatoi
ulinzi kwa raia wao.
Asubuhi
raia (Watoto, vijana, wazee) wakaamua kuwatolea uvivu askari na
kuandamana hadi kituo cha polisi kudai haki ya kulindwa na kuishi raia
walikua wengi kuliko uwezo wa askari wa kile kituo hivyo waliona hapa
wakiwa wakali kituo kitachomwa moto maaana walikuja na jazba raia
wakawaambia taarifa ziko kwa mkuu wa wilaya raia bila simile wakaanza
maandamano hadi kwa mkuu wa wilaya kufika huko naye akanawa mikono kama
pilato akasema mkuu wa mkoa ndo liko mikononi mwake.
Raia
hawakuishia hapo wakalianzisha hadi kwa mkuu wa mkoa huku wakiimba
"TUMECHOKA KUUWAWA" hadi kwa mkuu wa mkoa, hapo ndo movie ilpoanzia
kumbe raia wakati wanaenda kwa mkuu wa mkoa inaaminika simu zilipigwa
kwa mkuu wa mkoa na askari wanaolinda (FFU) wakafunga geti hapo ndo
ikawa vuta nikuvute raia wakaweka kambi nje huku wanaimba nyimbo "MKUU
WA MKOA UNAWAOGOPA RAIA WAKO JIUZURU", muda si mrefu gari ya FFU
likawasiri likiwa na askari wa kutosha kwa vile raia hawakua na silaha
wala ugomvi wakaamua kubaki huku wanaimba.
Askari
kama kawaida yao wakawa wanazidi kusogelea huku wakitoa ishara
wananchi watawanyike huku wananchi wakigoma hawatoki hadi mkuu wa mkoa
naye atoke nje hapo ndo askari wakaanza kufyatua risasi za moto na raia
wawili wakafa.habari zikafika mjini raia wameuliwa na askari hapo ndo
mji ukazizima raia wakaingia mitaani askari waliokua mitaani walianza
kupata upinzani mkali hd askari wawili wamekufa hadi hivi sasa, imebidi
jeshi liingilie kati na mji wote kufungwa hivi ss mjini ni makundi ya
wanajeshi na askari ndo yametawala hakuna maduka wala mabenki
yanayofanya kazi
Kutoka Mabadiliko .Chanzo;Mjengwa Blog
Kutoka Mabadiliko .Chanzo;Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment