- Ni kupitia promosheni ya tuma fedha kwa MPESA na ushinde
- 35 Milioni zaenda kwa wateja katika wiki ya kwanza
Wateja
700 wa Vodacom MPESA wamejishindia kiasi cha shilingi 35 Milioni
katika wiki ya kwanza ya promosheni ya tuma fedha kwa MPESA na ushinde
ilyozinduliwa wiki iliyopita ambapo jumla ya Shilingi 480 milioni
kushindaniwa.
Washindi
hao ambao kila mmoja amejishindia kiasi cha shilingi 50,000 katika
droo za kila siku. Mbali na droo ya kila siku promosheni hiyo
itachezesha droo moja kubwa kw akila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu
zitakazotoa washindi wa Shilingi 10 Milioni kila mmoja.
“Hadi
kufikia leo promosheni hii imeshatoa washindi mia saba, haya ni
matokeo ya mwitikio mzuri wa wateja wetu kushiriki na hii inatupa
faraja kwetumkwa kuwa lengo la Vodacom ni kuwafanya wateja wetu kuwa na
furaha watumiapo huduma yetu ya MPESA na kuwawezesha.” Alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza
Kupitia
droo hiyo washindi mia moja hujishindia shilingi 50,000 kila mmoja
ambazo mshindi huingiziwa moja kwa moja katika akunti yake ya MPESA.
.
Mwamavita
amesema huduma ya MPESA imekuwa sehemu muhimu katika maisha ya
wananchi ambayo imerahisha na kubadili maisha yao tangu ilipoanzishwa
Aprili, 2008, na hii inaenda sambamba na azma ya Vodacom ya kuthamini
mchango wa wateja wake kuunga mkono huduma hiyo kwa kuwawezesha na pia
kuifanya kuzidi kuwa huduma bora,salama,ya uhakika na rahisi..
“Ni
msimu mwengine ambapo tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufurahia huduma
bora,rahisi,salama na ya kuaminika ya Vodacom MPESA kwa gharama nafuu
zaidi sokoni kutoka kampuni inayoongoza soko la huduma za simu za
mkononi nchini. Alisema Bw. Rene katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari..
“Matumizi
ya huduma ya Vodacom MPESA yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana, na hii
inatufanya wakati wote kuongeza kasi ya kuifanya huduma ya MPESA
kuendelea kuwa huduma bora zaidi sokoni na yenye tija kwa wateja wetu
inayotoa huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi. Kadri mteja
anavyotuma pesa kwenda kwa mteja wa MPESA aliyesajiliwa au ambae
hakusajiliwa ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya juu ya kushinda
zawadi katika promosheni hii”Aliongeza Bw. Rene
Huduma
ya Vodacom MPESA ina mtandao wa mawakala zaidi ya elfu kumi na tano
nchi nzima na wateja zaidi ya milioni nane kati yao zaidi ya milioni
mbili wakifanya miamala – kutuma na kupokea fedha kwa kipindi cha mwezi
mzima mfululizo.
Kupitia
huduma ya MPESA mteja wa Vodacom aliyejisajili na huduma hiyo anaweza
kufanya manunuzi ama kulipia huduma mbalimbali za ikiwemo umeme – LUKU,
DAWASCO,DSTV,Muda wa maongezi, kuchangia michango ya harusi,kusaidia
misiba, ada, n.k ndani ya nchi na hata kutokea nje ya nchi.
Mbali
na promosheni hii wateja wa MPESA kwa sasa wanafurahia pia ofa
mbalimbali ikiwemo ya punguzo la asilimia 75 katika gharama za kutuma
fedha kwa MPESA mabapo sas amteja anatuma fedha kwa kiwango cha chini
kabisa cha shilingi 50 kuanzia shilingi 500 hadi elfu kumi, nyongeza ya
bonasi ya asilimia 25 mteja anaponunua muda wa maongezi wa hewani
kupitia MPESA.
No comments:
Post a Comment