Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin
Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu
uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini
Mbeya wakitembelea kiwanda cha
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni
mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini
Mbeya wakishindana kutambua ladha ya bia za kampuni ya Bia Tanzania
(TBL)
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), Edith
Mushi akimkabidhi katoni ya bia aina ya Castle Lager,
mwandishi wa habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Steve Jonas ambaye
alikuwa ni mshindi wa pili kati ya washindi watatu waliofanikiwa
kubaini ladha halisi ya bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo Jijini
Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo
Joachim Nyambo akipokea
zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na
Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka
mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na
kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa
huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.Picha Kwa Hisani Ya Full Shangwe
No comments:
Post a Comment