Usiku wa HIP HOP Ni Machi 4, 2012 Ndani ya Ukumbi wa Dar Live Jijini Dar es Salaam
Meneja Mkuu wa Global Publishers na Mratibu Msaidizi wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho akizungumza katika mkutano huo.
Profesa J akitoa vionjo katika mkutano wa leo.
Joh Makini naye akithibitisha kufanya makamuzi ambayo hayajawahi kutokea.
Wanahabari wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo.
Mapaparazi wakifanya kazi yao.Picha na Habari na Richard Bukos-GPL
--
Wadau
mbalimbali wa muziki wa Hip Hop hapa nchini, Jumapili ya Machi 4 mwaka
huu wanatarajiwa kufurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala
Zakhem jijini Dar es Salaam kuhudhuria onesho kabambe la Hip Hop.
Katika usiku huo wadau mbalimbali waliochangia muziki huu kufikia hapa
ulipo watatunukiwa tuzo. Wakali wa muziki huo Profesa J na Joh Makini
wamewawakilisha wasanii wenzao wa muziki huo katika mkutano wa
kuthibitisha kushiriki tamasha hilo uliofanyika mchana huu ndani ya
ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge jijini Dar.
No comments:
Post a Comment