Header Ads

Spika Wa Bunge Anne Makinda Ashiriki Mazishi Ya aliyewahi Kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu na Mshauri Mkuu wa Mambo ya Utawala wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania marehemu Leo Theodore Mnyanga

Viongozi wa dini wakijiandaa kwa ibada ya kumuaga aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali Watu na Mshauri Mkuu wa mambo ya Utawala wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania marehemu Leo Theodore Mnyanga aliyefariki dunia tarehe 22 Feb. 2012 na kuzikwa katika makaburi ya Mlima Kola nje kidogo ya mji wa Morogoro jana tarehe 26 Feb. 2012.
Wafanyakazi wa ofisi ya Bunge wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mnyanya kuelekea makaburini
Spika Makinda akiweka udongo kaburini.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaongoza waombolezaji kwa kutoa salamu za rambirambi katika mazishi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndugu Joel Bendera (kushoto), Spika Makinda na Mhe. Bura (kulia) wakimfariji mke wa marehemu (katikati). Picha zote na Prosper Minja -Bunge

No comments:

Powered by Blogger.