MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AZINDUA KAMPENI YA USAFI KATIKA MJI WA SUMBAWANGA LEO NA KUKABIDHI VIFAA VYA USAFI
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikabidhi vifaa vya usafi kwa
kikundi cha usafi cha Manispaa ya Sumbawanga kama sehemu ya Kampeni ya
usafi wa Mazingira katika Mji wa Sumbawanga.
Mama
Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais akifagia katika moja ya barabara za
lami katika Mji wa Sumbawanga kama ishara ya kuhamasisha wanawake
kushiriki kwenye usafi wa Mji huo.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la Msingi katika moja
ya barabara kuu za Mji wa Sumbawanga sehemu aliyozindulia Kampeni ya
usafi kwa Mji wa Sumbawanga. Kushoto ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu
wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal
akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya kushoto na Mama Asha Billal. Pembeni kushoto ni Mbunge wa Jimbo
la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
Makamu
wa Rais akiagana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed
Chima mara baada ya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa manispaa
ya Sumbawanga. Makamu wa Rais ameondoka leo Mkoani Rukwa na kuelekea
Mkoa jirani wa Mbeya ambapo atakuwa na ziara ya kikazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal
akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Kampeni ya usafi katika
Manispaa ya Sumbawanga ijulikanayo kama "Sumbawanga Ng'ara". Kampeni
hiyo ilianzishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa kwa nia ya
kuufanya Mji huo uwe wa mfano na wa kupendeza. Kushoto
kwake aliyeshikilia utepe ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya. Kampeni hiyo inaenda sambasamba na Kauli Mbiu ya "Dumisha
Usafi wa Mazingira, Dumisha Upandaji Miti na Dumisha Miundombinu
Daima".
Kwa hisani ya http://www.rukwareview.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment