Hali bado si shwari Songea, takribani 16 wadaiwa kuuwawa kikatili, wanyofolewa sehemu za siri
Na Mwandishi wa Thehabari.com, Songea
HALI ya
usalama kwa sasa ni tete katika Manispaa ya Songea kutokana na mauaji
ya kikatili ambayo yanaendelea kutokea mfululizo katika mji huo. Hadi
sasa takribani watu 16 wameripotiwa kuuwawa kikatili na maiti zao
kukutwa zimenyofolewa baadhi ya viongo hasa vya siri.
Usiku wa
kuamkia leo maiti nne zimeokotwa Manispaa ya Songea maeneo ya Paranyati,
Majengo, Matarawe na Mji Mwema, huku zote zikiwa zimeuwawa na
kutelekezwa ikiwa ni pamoja na kunyofolewa baadhi ya viungo vya mwili
hasa sehemu za siri.
Mauaji hayo yana husishwa zaidi na imani za
kishirikikina na watu hao huuwawa kikatili na kundi la watu
wasiojulikana, kisha kuchukua viungo vya sehemu za siri (yaani nyeti)
kama uume na uke, moyo na koromeo.
Shuhuda mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Jerome Komba akizungumza na Thehabari.com leo amesema
inadaiwa watu hao huchukuwa viungo hivyo na kuvipeleka nchini Msumbiji
kwa ajili ya masuala ya uchimbaji madini pamoja na machimbo ya madini ya
uraniamu eneo la Namtumbo.
“Yaani ndugu mwandishi hawa watu
wanataka utajiri wa haraka haraka na haya madini tuliyo nayo katika mkoa
huu (Ruvuma) yata tuponza,” anasema Komba.
Hadi sasa ni wiki ya
pili tokea matukio mfululizo yatokee. Kamanda wa Jeshi la Police Mkoa wa
Ruvuma, SSP-Naftari Matamba amekiri kutokea kwa matukio hayo katika
Mkoa wake hususani, Wilaya ya Songea na amedai polisi wanaendelea na
uchunguzi ili kuhakikisha watu wanaojihusisha na vitendo hivyo wanatiwa
nguvuni mara moja na kuchukuliwa hatua.
Taarifa zaidi zinadai Jeshi la Polisi Wilayani Songea limewapiga risasi na kuwauwa waandamanaji wawili wakiwa wanajitahidi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakitokea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Songea kuelekea Hospitali ya Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, kupinga matukio ya mauaji ya kikatili ambayo inadaiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa vyombo vya dola.

No comments:
Post a Comment