Waziri Nape avitaka vyombo vya Habari vya Serikali kuwa vinara wa ufichuaji wa maovu.

Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye akiwa anakazia
jambo kwa wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya TSN kuhusu
kuboresha kazi zao na kuandika habari zinazofichua maovu katika jamii na
kusimamia haki bila kumuonea mtu.

Mhariri
wa magazeti ya Daily News Bw.Charles Masele akimweleza jambo Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye(hayupo pichani)
mapungufu mbalimbali ya kampuni ya TSN na kumwomba waziri uyo awasaidie
kuiboresha kampuni hiyo.

Mwenyekiti
wa RAAWU tawi la Tanzania Standard Newspaper(TSN) Bw.Oscar Mbuza
akimweleza waziri Nape(kulia) changamoto mbalimbali ya wafanyakazi.

Sehemu
ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) wakimskiliza
Mhe. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye(hayupo
pichani).

Waziri
Nape nnauye akipiga “Selfie” na mfanyakazi wa magazeti ya kampuni ya
serikali ya TSN baada ya mkutano na wafanyakazi hao katika ofisi za
kampuni hiyo.

Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya Serikali(TSN) wakifurahia
picha ya pamoja na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape
Nnauye.Picha na Daudi Manongi.
……………………………………..
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewaasa
wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya Habari Leo,Daily
News,SpotiLeo na Sunday News kuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu
katika jamii,kwani kwa kufanya ivyo watajijengea heshima katika jamii na
kuongeza idadi ya watu kuwaletea kazi zao kwa ukaribu zaidi.
Waziri
nape ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam katika ofisi za
magazeti ya serikali(TSN) kwenye kikao na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Acheni
kumumunya maneno,msaidieni Rais katika kufichua maovu ya nchi yetu ila
tu msimuonee mtu bali mtende haki na hasa mkosoe ili kujenga na kwa
namna hiyo mtajijengea heshima kubwa katika jamii”.
Waziri
nape pia aliitaka menejimenti ya kampuni iyo kubadilisha fikara zao kwa
kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili kampuni iyo
ijitegemee vyema katika mambo yake.
Pia
aliitaka menejiment ya kampuni iyo kukaa chini na RAAWU ili wahakikishe
wafanyakazi wanafata taratibu za kazi na kuwaasa kushughulikia
vipaumbele vya wafanyakazi hao ambavyo ni vifaa vya kazi ambavyo
kutokuwa navyo inapelekea kushuka kwa morali ya kazi na pia madai ya
wafanyakazi yashughulikiwe ndani ya mwezi mmoja.
Nae
Mwenyekiti wa RAAWU katika kampuni iyo Bw.Oscar Mbuza alimweleza waziri
nape kuwa wanatambua haki na wajibu wa kila mfanyakazi na kwamba
kumekuwa na ukiukwaji wa sheria,taratibu na kanuni kwa mtizamo wao na
ivyo wanaomba yafanyiwe kazi ili kurudisha imani yao kwa viongozi wao.
Nao
wafanyakazi mbalimbali wa kampuni iyo walieleza changamoto
wanazokabiliana nazo ikiwemo kutokuwepo kwa bima ya afya,hawapandishwi
cheo na kulipwa malimbikizo mbali mbali wanayoidai kampuni hiyo.
Mhe.Nape
pia amehaidi kufanya vikao vya mara kwa mara na wafanyakazi wa kampuni
iyo ili kuboresha mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.
Story na Daudi Manongi.
No comments:
Post a Comment