WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI BANDARI YA MTWARA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya
ufisadi katika utoaji wa zabuni ya ujenzi wa gati mpya tatu.
Wazi
Mkuu ambaye alikagua eneo la ujenzi wa gati hizo jana (Jumamosi,
Februari 27, 2016), alisema anazo taarifa juu ya utolewaji wa zabuni
hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi
kupitia PPRA ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo.
Aliwaomba
wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi
wake uweze kuanza mara moja na kuleta ajira kwa wana Mtwara. "Ujenzi
ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta
mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka", alisema.
"Natambua
kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo
itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na
kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii
kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo
liko wapi," aliongeza.
"Sasa
hivi tuna uwezo wa kupaki meli moja tu, lakini gati zikikamilika
tutaweza kuwa na meli tatu kwa mpigo, cha msingi tusimamie maamuzi yetu
kwamba lazima wafanyabiashara wa korosho watumie bandari hii kusafirisha
mizigo yao na si kuipeleka kwingine."
"Kwenye
Bodi ya Korosho nako kuna majipu yanahitaji kutumbuliwa. RCC ilishakaa
na kupitisha uamuzi kuwa mizigo yote ipitie bandari ya Mtwara lakini
kuna watu ndani ya Bosi hiyo wanatoa vibali vya kusafirisha mizigo
kupitia bandari ya Dar es Salaam. "
Alimtaka
mkuu wa bandari ya Mtwara (Port Master) Bw. Prosper Kimaro awe makini
na watu wa kitengo cha manunuzi katika bandari hiyo kwani kimekuwa
chanzo cha upotevu wa fedha za Serikali kutokana na ujanja wa watu
wachache.
"Hapa
si kuna mtu alitaka kuiba sh. milioni 300 kwa kufoji saini za wakubwa
wake? alihoji Waziri Mkuu swali ambalo lilijibiwa na Bw. Kimaro kwamba
ni kweli lakini uongozi uliingilia kati kabla wizi huo haujakamilishwa.
Kuhusu
fidia kwa wakazi wa vijiji vya Kisiwa na Mgao ambao wamekubali kuhama
ili kupisha upanuzi wa bandari hiyo, Waziri Mkuu aliwahakikishia
wabunge hao pamoja na uongozi wa bandari kwamba kiasi cha sh. bilioni
13.8/- kimekwishatengwa na Wizara na kitatolewa mapema mwezi ujao.
Alitumia
fursa hiyo kusisitiza udhibiti wa bandari bubu ambazo zinatumiwa
kuingiza sukari na mchele mchezo ambao unaikosesha Serikali mapato.
"Mkuu wa Mkoa, nilikwishatoa agizo kama hilo wakati nimeenda kukagua
bandari ya Tanga. Kaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nanyi pia
muweke mbinu za kudhibiti upenyo huu wa kuingiza bidhaa za magendo kwa
sababu hawa ndiyo wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali," alisisitiza.
Naye,
Mkuu wa bandari hiyo, Bw. Kimaro wakati akitoa taarifa ya utendaji wa
bandari mbele ya Waziri Mkuu, alisema bandari hiyo ilianzishwa mwaka
1950 na imekuwa inakabiliwa na ufinyu wa gati ya kuegesha meli, vifaa
vya kupakulia na kupakia mizigo na kwamba hivi sasa wamekwishapata
winchi ya bandarini (harbour crane) yenye uwezo wa kubeba tani 100 na
tayari wako kwenye mpango wa kujenga gati moja.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.
No comments:
Post a Comment