WAMUOMBA MAGUFULI AWATATULIE TATIZO LA KIWANDA CHA MAFUTA KINACHO WACHAFULIA MAZINGIRA
Rais Magufuli akiwa anaongea na wananchi wa
eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la
Arusha
Na Woinde
Shizza,Arusha
Msafara wa
Rais John pombe magufuli uliokuwa ukielekea Monduli mapema leo umesimamishwa na wananchi katika eneo la Mbauda lililopo
ndani ya jiji
la Arusha ili kushinikiza kutatua kero zao
na changamoto zao ikiwemo kuwepo na
kiwanda cha mafuta ya kupikia
cha Mount Meru Mill kinachodaiwa kuchafua
mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Wananchi hao
ambao walijikusanya kuanzia mida ya saa mbili
kamili asubui mbali na kumueleza Rais huyo kero zao, pia walitumia nafasi hiyo
kumpongeza kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu
yaliyopo humu nchini.
Akiongea
mbele ya Rais mara baada ya kupewa nafasi , mmoja wa wanachi wa
eneo hilo la mbauda Thabiti Abubakari alimuomba rais awasaidie
kutatua tatizo la kiwanda hicho kutiririsha maji machafu ya
kiwandani kwani tatizo hilo ni baya na linawaharibia
mazingira na kuhatarisha afya zao .
‘’Musheshimiwa rais tunapenda utusaidie hapa kwetu mbauda
tuna kero kubwa inatusumbua, kuna hiki kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mount
meru mill kimekuwa kinatiririsha maji machafu ya kiwandani huku nje ambapo
wananchi wanaishi , kiwanda hiki hakijajenga mitaro
ya kupitisha maji machafu hivyo maji yote
machafu yakitoka huko kiwandani yanaingia huku majumbani kwetu, hivyo
muheshimiwa tunaomba utusaidie hili tatizo kwani kiwanda hiki kipo ndani ya
makazi ya watu,kinahatarisha afya sasa inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao
wanacheza uku mitaani pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama
kipindupindu maana maji haya ni machafu sana”alisema
Dhabiti
Akijibu swala
hilo Rais magufuli alisema kuwa amelisikia na aliwaagiza
mamlaka ya usafi wa mazingira nemc kulifuatilia swala hili
mara moja .
Aidha
magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa
jiji la Arusha kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwahaidi
ataendelea kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa akifanya
kampeni.
Alisema kuwa
kipindi hiki akuja arusha kwa ajili ya kuongea
na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi arusha kufanya mkutano
mkubwa ambao pia atatumia mda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji
la hilo.
No comments:
Post a Comment