Header Ads

KITAMBI NOMA YATWAA UBINGWA WA SOKA TAMASHA LA KWANZA LA AMANI NA UTALII

 

Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi kikombe cha ushindi wa bonanza la amani na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira.
wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha.
Na Woinde Shizza,Arusha

Klabu ya Kitambi noma ya jijini Arusha, juzi ilitwaa ubingwa wa soka
katika tamasha la kwanza la amani na utalii ambalo lilifanyika viwanja vya
General Tyre jijini Arusha.

Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuzishinda timu za Wazee Klabu na chuo  cha Uandishi wa habari Arusha(AJTC) kwa kukusanya alama nyingi kutokana na   mashindano yaliyoendeshwa kwa mfumo wa Ligi.

Katika tamasha hilo, liliandaliwa na taasisi ya Arusha media jumla ya timu
sita zilishiriki katika michezo mbali mbali na sambamba na kutolewa
burudani ya ngoma za asili kutoka kikundi cha Cultural Arts Center cha
chuo kikuu cha Makumira

No comments:

Powered by Blogger.