Watakaokwamisha juhudi za Rais Dkt. Magufuli katika sekta ya elimu kukiona - Masaju
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju akiongea na wazazi,
wanafunzi na Viongozi wa Shule za wanawake na wanaume za Feza katika
mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam na
kusisitiza katika umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.
|
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju akitoa veti kwa baadhi ya
wanafunzi waliofanya vizuri katika maaeneo ya Uongozi, Usafi na katika
Elimu katika kipindi cha miaka minne ya masomo yao.
|
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi na wahitimu wa kidato cha nne wa shule za Fedha.
|
Picha/Habari na Hassan Silayo
Wananchi
wameshauriwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano
za kuendeleza sekta ya elimu kwa maslahi na maendeleo ya watoto na nchi
kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju
wakati wa Mahafali ya Shule za Sekondari za Wavulana na Wasichana za
Feza Jijini Dar es Salaam.
Bw.
Masaju alisema kuwa anatambua Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe
Joseph Magufuli imeamua na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu
itolewe bure kuanzia ngazi ya awali (Kindergarten)
hadi kidato cha nne ikiwa ni njia ya kuwafanya watoto wa shule za
msingi au watoto waliofalu na kupata nafasi ya kusoma elimu ya sekondari
kutokusoma.
Masaju
alisema kuwa Asiwepo mtu atakayesababisha mtoto kukosa haki yake ya
kupata elimu kwa sababu yoyote ile ikiwemo kuwaozesha watoto, kuwapa
ujauzito, kuwaficha majumbani, kuwaachisha masomo, kuwatorosha shule,
utoro kwani kama nilivyoeleza awali kufanya hivyo ni kutenda kosa la
jinai chini Sheria ya Elimu na Kanuni zake hivyo serikali itachukua
hatua dhidi yake.
“Kama
tunavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe
Joseph Magufuli imeamua na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu
itolewe bure kuanzia ngazi ya awali (Kindergarten)
hadi kidato cha nne, hivyo asiwepo mtu atakayekwamisha juhudi hizi kwa
njia yoyote ile kwani ni kuwanyima watoto haki yao ya kikatiba kwani
Serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo” Alisema Masaju.
Pia
Bw. Masaju alizitaka shule na taasisi za elimu kutoa fursa sawa kwa
wanafunzi wote kutumia haki ya uhuru wa kuabudu kulingana na imani za
dini zao kwa kupanga mitihani au vipindi kwa muda au siku za kuabudu
kwani ni kukiuka masharti ya Ibara ya 19 inayotoa haki ya uhuru wa
kuabudu.
Aidha
Masaju alizipongeza sekta binafsi za elimu kwa kutoa mchango mkubwa
katika utoaji wa elimu hapa nchini kwa kuongeza wigo wa utoaji wa elimu
ya msingi na elimu ya sekondari; kuongeza vyanzo vya kodi na hivyo
kukuza uchumi na huduma za kijamii kutokana na kodi inayolipwa na shule
zinazotoa huduma ya elimu; kutunza na kuendeleza utamaduni wa Kitanzania
kwa kuwezesha watoto kusoma hapa Tanzania badala ya kupelekwa kusoma
nje ya nchi; na kuongeza ajira kwa walimu na watu wa kada mbalimbali
wanaoajiriwa na shule binafsi







No comments:
Post a Comment