ZANZIBAR YAANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELECTRONIKI KUSAMBAZIA DAWA NA KUPATA TARIFA ZA MADAWA VITUONI.
Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib
Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi
wa madawa jinsi unavyofanyakazi zake kwa haraka, katika hafla ya
uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini
Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la John Snow
Incorporated (JSI) nchini, Deo Kimera akitoa nasaha zake kwa Viongozi
na Maafisa wa Afya waliopata elimu juu ya matumizi ya mfumo mpya wa
Ugavi wa madawa wa kielektroniki walioshiriki katika hafla ya uzinduzi
wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna kushoto akihutubia mara baada ya
uzinduzi wa Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa
kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Hafla ya
uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini
Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mshauri Mwandamizi kutoka Shirika
la Misaada la Marekani USAID Kelly Hamblin akitoa shukran zake kwa
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano yao ya
kufanikisha Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa nchini,
katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel
Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid
Seif Suleiman akitoa shukrani zake kwa Shirika la John Snow Incorporated
(JSI) kutokana na juhudi zao za kuwawezesha maafisa wa Afya wa Zanzibar
kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa kwa njia ya
kielektroniki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park
Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mfamasia kutoka Bohari Kuu
Zanzibar Bi. Khadija Ali Shehe akielezea changamoto walizokumbana nazo
wakati wa kutumuia mfumo wa Karatasi katika Usambazaji wa Madawa
vituoni kabla ya kuzinduliwa Mfumo mpya wa kielectroniki hii leo.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya
Gombani Pemba Abdalla Mbaruk Saleh akitoa ushuhuda wa namna Mfumo mpya
wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa unavyofanya kazi zake kwa haraka na
ufanisi, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt
Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna katikati akizindua Mfumo mpya wa
Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa
Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Kulia kwake ni Msimamizi wa taaluma
kutoka Shirika la John Snow Incorporated (JSI) Anselm Namala ,na
kushoto ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman. Hafla ya uzinduzi wa
mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.








No comments:
Post a Comment