Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama,
vijana na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni
ya kujionea namna bora yautoaji huduma. Mama Salma yupo nchini
Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya
kiserikali nchni humo.
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete
na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama
Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea
maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika
hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na
wazazi wao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akimpa pole na kumtakia apone haraka binti Addison Stephen,6,
aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa hospitalini hapo
huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen Miles (aliyesimama
kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Mama
Elizabeth Chatham.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri wa siku moja aliyezaliwa na
uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali ya Caniberra nchini
Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34, na Bibi Tania
Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi jarida
linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi
Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto ya Caniberra nchini
Australia mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbaali za kutolea huduma
hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali wa Australia Mama
Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na Gavana Generali wa nchi
hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe
28.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu ya Australia huku Rais Dkt.
Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe
wakishuhudia.
PICHA NA JOHN LUKUWI.








No comments:
Post a Comment