POLISI ARUSHA KUWAFANYIA USAILI ASKARI WATARAJIWA

Na woinde shizza,arusha.
Jeshi la Polisi
Mkoani hapa linatarajia kuwafanyia usaili vijana wa Mkoa huu waliomaliza kidato
cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kupitia tovuti ya Tamisemi
ambayo ni www.pmoralg.go.tz.
Wanaotarajia
kujiunga na mafunzo ya Jeshi
la Polisi.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus
Sabas aliyasema hayo ofisini kwake leo asubuhi ambapo alisema zoezi hilo
litafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 06.07.2015 na
tarehe 07.07.2015 katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi za Mkoa
huu.
Aidha alisema zoezi
hilo litaanza kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni huku tayari majina
ya vijana waliochaguliwa na maelezo yake yameshabandikwa katika ofisi za Mkuu
wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha na
Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa wilaya ya Arusha Mjini huku wilaya za
Longido, Arumeru, Monduli, Karatu na Ngorongoro majina yao yatabandikwa kwenye
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri husika za wilaya
hizo.
Waombaji watatakiwa
wawe na vyeti vyote vya masomo (Academic Certificate(s)/Result Slip(s) &
Leaving Certificate(s) na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (original Birth
Certificate) huku Hati ya Kiapo cha kuzaliwa haitakubaliwa pia atatakiwa kuwa
na namba za simu ambayo itasaidia kumjulisha endapo atachaguliwa.
Aidha Kamanda Sabas
alisema kwamba kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri,
chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili huku atatakiwa kuwa na
kalamu ya wino kwa ajili ya usaili wa kuandika bila kusahau kuzingatia tarehe
na muda kuanza usaili.
Kamanda alimalizia
kwa kusema kwamba, Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo
chochote
cha usaili kilicho karibu naye ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa
walioitwa kwenye usaili.
No comments:
Post a Comment