Header Ads

NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI 570

 Mkuu wa Wilaya  ya Busega Mkoani Mwanza Bw. Paulo Mzindakaya , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kulia), baada ya kukabidhi  madawati 240 yenye thamani ya shilingi milioni .... yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Nyashimo na Nasa Wilayani Busega pamoja na Sukuma na Simakitongo Wilaya ya Magu ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati sitini.
 Mkuu wa Wilaya  ya Musoma Mkoani Mara Bw. Zelothe Stephen , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto), baada ya kukabidhi  madawati 330 yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Bwai, Kiriba, Chanyahuru na Busumi pamoja na shule ya Sekondari Kiriba zilizopo Musoma vijijini ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati hamsini na tano.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB

No comments:

Powered by Blogger.