NHC yanyang’anya mashine za kufyatulia matofari baada ya Halmashauri za Mikoa baada ya kushindwa kutumia fursa hiyo
● Mkoa wa Katavi na Rukwa washindwa kutumia fursa ya msaada huo
● NHC yanyang’anya mashine Halmashauri za Mikoa hiyo
● Zatakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara
Katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatunzwa, kutumika
ipasavyo na kuhakikiwa, NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa
msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi
kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya
Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa.
Kwa
ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji
msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na
mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya
kuuzia wananchi. Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya
hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana
mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo
ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo.
Hata
hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo
ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana
na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na
kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo
kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana
wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
Kikundi
cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna
ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi
alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana
hao wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza
kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.

Hii
ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa
Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa
vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo
ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa
Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri,
kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa
kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa
vikundi vya awali vilundwa kisiiasa.

Kikundi
cha vijana cha ITIMBA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
Vijijini kikimsikiliza` Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano
Kasibi Saguya alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili.
Kikundi hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea
majengo mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza. Halmashauri
ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo
ya kufanyia kazi.

Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bw. James
Milanzi akimsikilza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano
Saguya alipofika Ofisini kwake kukumbusha wajibu wa Halmashauri za
Wilaya wa kusaidia vijana ili waweze kutengeneza matofali ya kujengea
nyumba za gharama nafuu na kujipatia ajira. Halmashauri hiyo imepiga
marufuku ukataji miti kwa ajili ya kuchoma matofali na badala yake
wananchi wametakiwa kutumia matofali rafiki wa mazingira yanayozalishwa
kwa kutumia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana katika
Halmashauri zote nchini.
No comments:
Post a Comment