ZIARA YA KATIBU MKUU NDANI YA JIMBO LA MAGU LEO,KESHO KURINDIMA JIMBO LA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza
Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao
aiyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Magu,Bi. Juliana
Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.Zaidi ya
wananchama 53 kutoka vyama vya upinzani walijiunga na CCM wakiwemo
Chadema 28 na ACT 12 na wengine kutoka vyama vingine.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi.
Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni
Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akionyesha kadi zilizokuwa za wanachama wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu
mkoani Mwanza.
Katibu
Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA
(BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha
Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa
wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini na
nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.
Kinana amesikiliza kero mbalimbali
za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia
katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye .

Baadhi ya Kadi za wafuasi wa vyama mbalimbali walizoamua kuachia ngazi na kuhamia chama CCM.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu
Magesa Mulongo wakifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa utumiaji wa
maji hayo katika mji wa Magu.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu. Katika Kikao hicho Katibu Mkuu wa
CCM amewajia juu Viongozi wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kujifanya
maarufu zaidi ya Chama alisema "Hakuna mtu maarufu zaidi ya CCM huku
akisema kuna watu wanaona kama wamekiteka hiki chama nyara na kukiweka
kwenye kikapu na kuzunguka nacho, Hatutokubali hilo litokee" aliendelea
kusema bora mtu aende upinzani kulikoni kuwa na sisi halafu anatuumiza.

Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu
kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda
katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za
uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya
moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana
kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Magu
mjini,aliyekuwa akitoa kero yake kubwa ya upatikanaji wa maji katika
eneo hilo,katika mkutanno wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa saba
saba

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa
na baadhi ya wakazi wa mji wa Magu mapema leo jioni katika mkutanno wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa saba saba

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofari mara baada ya
kushiriki kufyatua wakati alipokagua shughuli za kikundi hicho katika
kijiji cha Irungu wilayani magu.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akzungumza jambo mara baada mara baada ya
kukabidhi mashine kwa vijana wafyatua matofali katika kijiji cha
Nyigoro-Ilungu wilayani Magu,ambapo vijana hao walipata tenda ya
kujenga Nyumba
ya Bibi Asteria Selemani inayojengwa na Mwanaye Zakaria Andrew katika
kijiji cha Irungu wilayani Magu Anderw amekipatia tenda ya kufyatua
matofali ya kujengea nyumba hicho kikundi cha vijana ambacho
kimefadhiliwa mashine ya kufyatua matofali na Shirika la Nyumba
Tanzania NHC.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa
Mhandisi wa maji wa Wilaya ,Injinia Rutta Merchades alipotembelea chanzo
cha maji Nyanguge wilayani Magu.

Wakazi
wa Nyanguge wakisubiri maji kuzinduliwa na katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya mkoa wa Mwanza ya kukagua
,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa Maji Nyanguge.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji kama
ishara ya kuzinduliwa kwa huduma za maji Bi.Yustina mkazi wa Nyanguge.


Pichani ni moja ya jengo la X-Ray linalojengwa katika kituo Afya Kisesa wilayani Magu.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Kisesa mapema
jioni ya leo alipokuwa akimaliza ziara yake ndani ya jimbo la Magu.
No comments:
Post a Comment